Ndalichako kumaliza migogoro ya walimu kwa kushirikiana na wizara nyingine

February 19, 2017

  Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13 uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)
Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
 Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Djibouti, Mh. Moustapha Mohamed Mahamoud akiwasilisha mapendekezo ya serikali yake katika kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde (kulia) akitoa mapendekezo ya serikali yake katika kuboresha elimu kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mh. Mhandisi Stella Manyanya (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo wakiandika mapendekezo muhimu yaliyokuwa yakiwasilisha kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Sehemu ya mawazi wa elimu kutoka Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti walioshiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
  Sehemu ya wadau wa sekta ya elimu kutoka nchi 13 walioshiriki kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akifuatilia mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiwasilishwa na wadau wa sekta ya elimu wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) walioshiriki kufanikisha mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo (kushoto) akijadiliana jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Da es Salaam.


Na Zainul Mzige
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine nchini kuhakikisha kwamba migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha utoaji wa elimu kuwa bora na jumuishi.
Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya pili ya kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika Mashariki kujadili lengo la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs)
Alisema kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na mazingira bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na kusema kwamba wao kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni kuzungumza na wenzao kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili utoaji wa elimu uendane na mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la maendeleo 2030.
Pamoja na kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia  kwamba walimu walikuwa ni ajenda muhimu  na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila kitu katika utoaji wa elimu na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu bora na jumishi bila kuwa na walimu wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya hivyo.
Kutokana na ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.
Alisema kila nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba vinatekelezwa kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote yanapaswa kuhakikisha kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya elimu imetekelezwa.
Alisema katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank wamebainisha kwamba mikakati ya pamoja ni lazima ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi yenye usawa na ubora kwa watu wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.
Alisema kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa na mfumo wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami kutokana na kubadilika kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina budi kujazia nafasi hiyo kwa kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.
Alisema nchi hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030 kama yalivyosainiwa na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili mataifa hayo yaweze kufikia malengo yanayotakiwa.
Aidha alisema kama walikubaliana kwanza kuimarisha elimu ya awali kwa lengo la kuweka msingi wa kujifunzia, kwani ipo methali inayoaminika kwamba samaki mkunje angali mbichi na taifa likitaka watoto wasome ni lazima kuwaanzia wadogo.

Aidha  mataifa hayo yamekubaliana upimaji wa wanafunzi kufanyika kwa ajili ya kujifunza, ukilenga kutumia matokeo kuandaa mafunzo kwa wanafunzi. Upimaji uoneshe eneo la ambalo walimu watalazimika kufanya kazi ya ziada ili wanafunzi wao waelewe.
Mfumo wa sasa wa kupima umelenga kujua watoto wangapi wamefaulu na wangapi wamefeli.
Ndalichako alisema ni vyema upimaji huo kutumika kuimarisha mafunzo ya walimu.
Jambo la tatu ambalo walikubaliana ni kuhakikisha kwamba mtoto wa kike anasoma na wale wenye mazingira hatarishi pia; na bila kujali kujali mazingira yao nchi zinatakiwa kuweka mikakati ya  elimu iliyobora kwa wote.
"Suala muhimu katika elimu ni kupanga mipango sahihi. Takwimu sahihi ni changamoto kutokana na ukweli kuwa takwimu hazipatikani kwa wakati au hazina usahihi au hazifanyiwi uchambuzi katika kufanya maamuzi vizuri, " alisema Prof Ndalichako.
Pia mataifa hayo yakiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia, Comoro na Djibouti yamesisitiza haja ya kuimarisha elimu nje ya mfumo rasmi na kwa kuwa kuna mfumo wa elimu wa kujiendeleza wa wakati wote mfano wa uhasibu.
Alisema inafaa kuimarisha mifumo ya elimu nje ya mfumo rasmi bila kusahau elimu ya watu wazima. Pia wametaka watoto wanaolikoroga kwa sababu moja au nyingine na kujikuta hawapati masomo ni vyema wakarudishwa shuleni kuendelea na masomo hivyo ipo haja ya kutengeneza mfumo wa kupata elimu kwa staili hiyo.

"Katika hili tumekubaliana watoto walionje ya shule wanarudi shuleni au wanatengeneza mfumo wa kupata elimu" alisema na kuongeza kuwa pia ilionekana ipo haja ya kuimarisha elimu na ufundi stadi ili elimu hiyo imwezeshe kujiajiri, kujijenga na kuwa na ujuzi kuendana na soko la ajira.
Aidha alisema kwamba  kunatakiwa kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kufichua wasichana wasiopelekwa shule ili kuwepo mwenedelezo wa kila mtu kuingia shule.
WAKATI huo huo serikali ya Uganda imesema itaongeza nguvu katika shule za awali kuimarisha msingi wa utoaji elimu kwa watu wake.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu na shule za msingi wa Uganda, Mh. Nansubuga Rosemary Seninde wakati akizungumza katika mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki kuhusiana na lengo namba 4 la elimu kati ya malengo 17 ya dunia.
Alisema serikali yake imejikita katika kuhakikisha kwamba waganda wanapata elimu nzuri na yenye ushindani ikihakikisha ujuzi na uzoefu katika ujuzi.
Aklisema nchi yake haiwezi kumpa mtu digrii mpaka awe amefanya “intern” na hilo linasaidia sana kujenga uzoefu wa kile alichosomea.
Alisema ingawa kuna tatizo la bajeti, mipango ni muhimu kuhakikisha kwamba taifa linatoka katika changamoto za utoaji wa elimu bora.

Alisema badala ya kusubiri sera, watendaji wanatakiwa kuangalia maeneo ya kuanzia na kisha kutengenezea taratibu za kubadilishwa kwa sera ili iendane na kasi inayotakiwa.
-- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »