Na,Abel Daud,Globu ya Jamii- Kgoma.
Katika
kuepuka vifo vya mama wajawazito na watoto,wazazi wameshauriwa
kutotumia dawa za asili sambamba na kuwahi kufika katika vituo vya afya
ili kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto.
Rai
hiyo imetolewa na Daktari mfawidhi wa kituo cha afya Nguruka
Dkt.Stanford Chamgeni ,wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza
Bi,Mwanamvua Mlindoko katika kukabidhiwa jengo la maternity ward
lililopo katika kijiji cha Mganza kata ya Mganza Wilayani Uvinza lenye
dhamani ya tsh.30 million,lililotolewa na Kanisa la POOL OF SLOAM.
Naye
Kuhani ISRAEL EXTRA POWER,ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa
hilo hapa nchini,alisema kuwa kupitia hatua hiyo ni sehemu ya kuunga
mkono jitihada za serikali katika kukamilisha huduma za kijamii.
Akinukuu
maneno ya kitabu cha Isaya 58 aya ya 7 na Yakobo 2-14,Kuhani ISRAEL
POWER alieleza kuwa,sehemu ya kusaidia maisha ya wenye uhitaji lazima
kuwepo na umoja kwa viongozi na jamii kwa ujumla,sambamba na kuongeza
kuwa,kwa kuwa MUNGU hana upendeleo,kama kanisa ni lazima kuendelea kuona
uchungu wa kuhudumia jamii.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Mganza Bw,BONIFACE BAHINGAI,ametoa
shukurani kwa kanisa hilo ambapo alisema kuwa kuwepo sasa kwa ward
hiyo,itasaidia kutatua changamoto zilizokuwepo kijijni humo,sambamba na
kutoa wito kwa taasisi zingine za kidini kuona umuhimu kusaidia huduma
za kijamii.
Nao
baadhi ya wananchi kijijini humo akiwemo DAFROZA GWIMO,alitanabaisha
kuwa uwepo sasa wa ward hiyo itawarahisishia kuondoa changamoto
iliyokuwepo ya kwenda kujifungulia mbali,na kupelekea kuhatarisha maisha
ya mama mjamzito na mtoto.
Waumini wa kanisa hilo pamoja na wanakijiji wakiwa wamelizunguka jengo hilo
Kuhani Israel Extra Power akiongea na wana kijiji pamoja na waumini waliohudhuria sherehe hiyo
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya pamoja na Kuhani Israel Power wakielekea kwenye jengo tyr kwa uzinduzi
Kuhani Israel Power akimkabidhi ufunguo wa jengo hilo Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya Dr.Chamgeni
Kuhani Israel pomoja na Dr.Chamgeni wakifunua kitambaa kilichofunika jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa jengo hilo
EmoticonEmoticon