Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Yemen nchini Mhe.Fikri
Taleb Abubaker Al Sakaf mara baada ya kuwasili Wizarani kuwasilisha
Nakala za Hati za Utambulisho
Mhe.
Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionesha Hati za Utambulisho za
Balozi Mteule wa Yemeni nchi Tanzania Mhe.Fikri Taleb Abubaker Al Sakaf
mara baada ya kukabidhiwa
aziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Saudi Arabia nchini
Tanzania Mhe. Mohammed Bin Mansoor Al Malyk alipowasili Wizarani Jijini
Dar es Salaam kukabidhi Hati za Utambulisho
Balozi
Mteule wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Mohammed Bin Mansoor Al
Malyk akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri Balozi Dkt.
Augustine Mahiga Wizarani Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Malawi nchini
Tanzania Mhe. Hawa Ndolowe alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam .
Mzungumzo
yakiendelea, Kushoto ni Balozi Msaidizi wa Malawi nchini Tanzania
Bw.Sai Kaphale na Kulia ni maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia
mazungumzo yalikuwa yakiendelea.
Wakiwa katika picha ya pamoja
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akimsikiliza Balozi wa Japan nchini Tanzania
Mhe.Masaharu Yoshida alipomtembelea kwa mazungumzo yaliyofanyika
Wizarani Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo
yakiendelea. Kushoto ni Maafisa kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania
na kulia ni Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa
yakiendelea .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (Mb), amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Waheshimiwa
Mabalozi Wateule wa Nchi za Yemen na Saudi Arabia na baadaye kufanya
mazungumzo na Waheshimiwa Mabalozi wa Malawi na Japan leo ofisini
kwake.
Wakati
wa mazungumzo na Balozi Mteule wa Saudi Arabia, Mhe. Mohammed Mansour
Al-Malik viongozi hao walisisitiza umuhimu wa Tanzania na Saudi Arabia
kuimarisha uhusiano na ushirikiano hususan katika nyanja za biashara na
uchumi. Dkt. Mahiga alimweleza Balozi Mteule kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alifurahishwa
na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al
Jubair aliyoifanya nchini mwezi Machi 2016.
Wakati
wa ziara hiyo, Rais Magufuli aliomba Serikali ya Saudi Arabia kupitia
Mfuko wa Serikali (Saudi Fund) kufadhili ukamilishwaji wa miradi
mbalimbali ya barabara hapa nchini. Ombi hilo liliafikiwa na ujumbe
kutoka Saudi Arabia ulifanya ziara nchini hivi karibuni kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi hiyo.
Rais
Magufuli pia alitumia fursa hiyo kumualika Waziri wa Mambo ya Nje wa
nchi hiyo kutembelea Hifadhi za Taifa zilizopo hapa nchini. Mhe. Waziri
alikubali isipokuwa alisema atakuja wakati mwingine na mwanae wa kiume
ambaye anapenda sana kuona paka wakubwa akimaanisha wanyama wakubwa kama
simba, chui, tembo na faru.
Kwa
upande wake, Balozi Mteule wa Saudi Arabia aliahidi kusimamia
utekelezaji wa yote yaliyoafikiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya
Nje wa nchi yake na masuala mengine yenye maslahi ya pande zote mbili.
Wakati
wa mazungumzo na Balozi Mteule wa Yemen, Mhe. Fikri Taleb Abubaker
Al-Sakaf, wawili hao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya
nchi hizi mbili. Waziri Mahiga alitumia fursa hiyo pia kuwaalika
wafanyabiashara wakubwa kutoka Yemen kuja kuwekeza Tanzania. Alisema
kuna wafanyabiashara wengi wenye asili ya Yemen wamefanikiwa kibiashara
hapa nchini.
Aliongeza
kuwa historia inaonesha kwamba watu kutoka Yemen ndio walikuwa wa
kwanza kufanya biashara za maduka ya bidhaa muhimu nchini ambao walikuwa
na utaratibu wa kukopesha bidhaa na kulipa baadaye. Alisema watu hao
kutoka Yemen pia ndio walikuwa na utaratibu wa kupeleka bidhaa hadi
vijijini na kukopesha wateja wao ambao leo unatumiwa na wafanyabiashara
wa Tanzania kwa jina maarufu wamachinga.
Kwa
upande wake, Balozi Mteule wa Yemen aliahidi kuwa atafanya kila awezalo
kushawishi makampuni makubwa kutoka Yemen kuja kuwekeza nchini. Alisema
kama watu wa Yemen walikuwa wanafanya biashara ndogo ndogo huko nyuma
hapa nchini, kuna haja sasa ya kupanua wigo na kuingia katika biashara
kubwa.
Wakati
wa mazungumzo na Balozi wa Malawi, Mhe. Hawa Ndilowe, wawili hao
walisisitiza pia umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi
mbili. Aidha, Mhe. Ndilowe alimweleza Waziri Mahiga kuwa Malawi
imejipanga kuandaa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano
kati ya Tanzania na Malawi (JPC) mwezi Desemba 2016. Alieleza mara ya
mwisho kufanyika mkutano huo ilikuwa mwaka 2003 nchini Tanzania, hivyo
kuna umuhimu wa kuitisha mkutano huo ili kutoa fursa kwa wadau kujadili
masuala mbalimbali ya ushirikiano pamoja na kutafuta mbinu za
kukabiliana na changamoto zinazotukabili.
Waziri
Mahiga alikaribisha uamuzi huo kwa furaha kwa kusema kuwa wakati wa
mkutano huo itakuwa fursa nzuri ya kufafanua masuala mbalimbali ambayo
yamefanyiwa mabadikiko na Serikali ya Awamu ya Tano, hususan katika
sekta ya usafirishaji katika Bandari ya Dar es Salaam, mifuno ya ulipaji
kodi, uhamiaji na biashara za mipakani.
Aliendelea
kueleza kuwa Tanzania na Malawi zinatakiwa kushirikiana katika masuala
ya ulinzi na usalama, hususan katika kukabiliana na mauaji ya watu wenye
ualbino ambayo yameikumba nchi zao.
Katika
mazungumzo yake na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe. Masaharu Yoshida,
Waziri Mahiga alipongeza ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi mbili
ambao umejikita katika kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu
hapa nchini kwa ajili ya maendeleo.
Aidha,
akitoa maoni yake kuhusu Mkutano wa Sita wa Kimataifa kuhusu
Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Japan na Afrika (TICAD VI) uliofanyika
kwa mara ya kwanza Afrika, Jijini Nairobi mwezi Agosti, 2016, Waziri
Mahiga alisema mikutano hiyo ni jukwaa muhimu linalotoa fursa kwa nchi
za Afrika na Japan kujadili maendeleo.
Pia alipongeza agenda zilizojadiliwa kwenye mkutano wa TICAD VI ikiwemo kuhamasisha
mageuzi ya kiuchumi kupitia uendelezaji wa viwanda; Kuboresha sekta ya
Afya kwa maisha bora na kusaidia jitihada za kudumisha amani na utulivu
katika jamii kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 17 Novemba, 2016.
EmoticonEmoticon