HII NI KWA AJILI YA VIJANA WOTE JAPO WAZAZI NA WALEZI WANARUHUSIWA KUSOMA.

November 17, 2016

Ujana ni ngazi ambayo inahitaji umakini mkubwa katika ngazi zote za maisha mwanadamu (maoni binafsi).

Ni kipindi ambacho asilimia kubwa ya vijana hufanya mambo ili waonekane na jamii inayowazunguka.

Ni wakati ambao wengi hupoteza muda na mwelekeo wa maisha yao kwa sababu, asilimia kubwa hufanya mambo kwa kufuata mkumbo. 

Wengi hupotea maana ni muda ambao huanza kuwa na maamuzi binafsi. Hapa wazazi na walezi wakijitenga kando, kijana huangamia maana wengi huchagua maovu kuliko mema. 

Kama hujaanza mahusiano, utaanza kwa sababu yule ameanza. Hata kama huna kazi nzuri, utaanza kubagua kazi kwa sababu fulani ana kazi nzuri. Ulevi na uzinzi huanzia katika ngazi ya ujana. Inasikitisha.

Hayo ni machache miongoni mwa mambo mengi ambayo hukatisha mafanikio ya vijama (Me & Ke).

Mimi nasema utumie ujana wako vizuri leo ili kesho usijutie. Najua peke yako huwezi hivyo kaa chini, tafakari, kisha chagua dini ya kweli inayokufaa, kisha anza maisha yako ya ujana ukiwa na mahusiano mema na Mungu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »