MAKALA YA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI

November 17, 2016
Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi


  Na  Walter  Mguluchuma wa Katavi yetu Blog
   
  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  inapatikana  kusini  Magharibi  mwa  Tanzania   karibu na  Ziwa  Tanganyika   katika  Wilaya za  Mpanda  ,Tanganyika  na  Mlele    Mkoa wa  Katavi  inapatikana  katika  latitude 6.63.7.34 kusini na   na  longitude  3.74.31.84  Mashariki.

  Hifadhi  hii  ilitangazwa  kuwa  Hifadhi ya  Taifa   mwaka 1974 ikiwa  na  ukubwa  wa  kilometa za   mraba  2253 iliongezwa  ukubwa  mwaka  1996 na kufikia  ukubwa  wa kilometa za  mraba  4471 na kuifanya kuwa   Hifadhi  ya tatu  kwa ukubwa  Tanzania  baada ya Ruaha na   Serengeti .

 Ilipata  jina   lake  kutokana  na  mzimu  wa  kabila la Wabende  aliyejulikana kwa  jina  la  Katabi  ambapo mpaka  leo watu  mbalimbali  wamekuwa wakifika ndani ya  Hifadhi ya  Katavi na kwenda  kwenye  mti  ulioko  kwenye  Ziwa  Katavi  wakiamini kuwa  mzimu  Katabi alikuwa  akiishi  hapo  zamani   kabla ya kuwepo  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi .

Jina la  Hifadhi hii  lilijulikana   kama   Katabi  kutokana  na imani  ya  jamii   hizo kwa  mzimu  Katabi  inaaminika  kwamba  mzimu  Katabi  una uwezo  wa  kufanya miujiza  ikiwemo  kufanya mvua  inyeshe , kuzuia  magonjwa  ya mlipuko  kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
Hifadhi hii  inafikika  mwaka mzima  kwa kupitia  Mikoa ya  Dares,salaam,Mwanza , Kigoma   Arusha     hadi  Mpanda  kupitia  Tabora kwa kutumia  usafiri wa  ndege  za kukodi    Chartered planes  au kwa njia ya  barabara kwa kupitia  Mbeya   na  Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa  Treni kutokea  Tabora .

Katavi   'National  Park'  inawanyama wengi na  adimu  na wakubwa kuliko  wanyama  wanaopatikana  kwenye  Hifadhi  nyingine  hapa   Nchini  kutoka  na  hari ya uoto wa  asili  uliopo  kwenye   Hifadhi hii ambayo kwa sasa imeanza kupata watalii tofauti na  hapo  awali .

Mbali ya kuwepo  kwa  wanyama  wengi   madhari yake ni  pana  kuanzia  uwanda  tambarare wa  nyasi  katika  mkondo  wa  bonde  la ufa   hadi  kwenye miteremko  mikali  ambayo ni  matawi  mawili  sambamba na bonde la ufa la    Mashariki   maarufu  kama  bonde la ufa la   Rukwa .
Uoto uliopo unavutia  unavutia sana kuanzia  kuanzia  Misitu  iliyofunga  mpaka misitu ya wazi  ,vichaka  uwanda wa  nyasi  maziwa  ya msimu ya   Chada  na  Katavi  mabwawa na uoto  kando ya mito .

 Wakati wa kipindi cha  mvua  kuna   aina  nyingi za  maua   aina ya  'species' mbalimbali  za miti na majani  aina za  'species' 226 za miti zimeisha tambuliwa  zikiwemo  aina  tatu   zenye   mvuto  wa kisayansi .

  Uhai  wa  Hifadhi  ya  Katavi  unategemea  mto  Katuma   ambao  humwaga  maji  yake   ziwa   Katavi  upande wa  kaskazini ,Ziwa  Chada  na  mbuga  yenye  eneo la  kilometa za  mraba  425 ambayo  hutuamisha   maji  Floodplain katikati ya  Hifadhi  ziwa   Chada  hupokea  pia  maji  kutoka  mto  Kapapa   ambao  mkondo wake  hutokea   Kaskazini  mwa  Hifadhi ya  Taifa   Katavi .

  Kuna  aina  mbalimbali  za   wanyama pori ,idadi  kubwa  ya vipepeo  na  ndege  wa   aina   mbalimbali  katika  Hifadhi ya   Katavi  ni kivutio  vikubwa  kwa wageni   idadi ya   watalii  na   shughuli za   maendeleo    ndani ya   Hifadhi   bado ni   ndogo   hivyo  kufanya  mazingira  kuwa  asilia  zaidi .

Baadhi ya  wanyama  wanaopatikana  kwenye   Hifadhi ya    Katavi  ni  makundi  makubwa ya   Tembo ,  Nyati,  Simba ,  Pundamilia ,  Mbwa  mwitu ,  kongoni  Swala  pala ,   Nyemela  na  wanyama  wengineo .

Pia  kwenye  eneo la  mto   Stalike  na   Iku  utakuta  kuna  makundi makubwa  sana ya  viboko na  mamba  ambapo kumekuwa na  mapigano  ya  mara kwa  mara  na  kufanya  eneo hilo kuwa  kivutio kikubwa kwa watalii.

Upande wa   Hotel  hifadhi hiyo  inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya  Hifadhi  iiingawa  bado  ni  chache  pia   hotel nyingine   zinapatikana   katika   Kijiji cha  Stalike  ambacho kipo  jirani na  Hifadhi  na  pia   katika   Mji wa  Mpanda        makao  makuu ya  Mkoa wa Katavi  uliopo  umbali wa kilometa   40 kutoka   Hifadhi ya  Katavi .

 Hivi  karibuni   kaimu   Mkuu wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi    Elias   Manase  aliwaambia   wandishi wa  Habari wa  vyombo  mbalimbali wa   Mkoa wa  Katavi  kwamba  Hifadhi  hiyo  inakabiliwa  na   changamoto  mbalimbali .

Baadhi ya   changamoto hizo ni   ujangili   wa  wanyama  hasa  Tembo   ambao  unasababishwa na kuwepo kwa  kambi za wakimbizi   za    Mishamo na  Katumba  ambazo wanaishi  Raia wa  Burundi na  Kongo .

  Ilidai   kuwa  watu wanao ishi kwenye  makazi  hayo wamekuwa  wakiingiza   silaha za  kivita  na kuziingiza  nchini kisha wamekuwa wakifanya ujangili wa kuuwa  Tembo  na kisha  wanachukua  meno ya  Tembo na kuyasafirisha  kwenye  soko  la  nchi  jirani.

Changamoto  nyinginei ni  uhaba wa miundo  mbinu  ndani ya   Hifadhi kwani  bado  haiku  mizuri  sana  ingawa   barabara  zake zinapitika  karibu  mwaka  mzima .

Manase  alitowa  wito kwa  watanzania  kujenga utamaduni wa kutembelea  Hifadhi za Taifa kwani   gharama ya kutembelea  Hifadhi  za  Taifa ni  ndogo kuliko  gharama ya  mtu  anayoitumia  kwenye   Bar  kunywa  pombe . 

Askari wa   Hifadhi   ya  Katavi  Joseph  Mhina aliielezea  Hifadhi ya  Katavi  kuwa     ni   hifadhi  ambayo  ipo  tofauti     kabisa  na  Hifadhi  nyingine kwani  watalii wanaotembelea   Hifadhi  hiyo  huwa  wanawaona wanyama kiurahisi  kabisa kwani  watalii  huwa ni wachache hivyo   huwa   hakuna kugombania kuwaona  wanyama  kama  Hifadhi  nyingine .

Imeandaliwa na Blogs za Mikoa kupitia Katavi yetu Blog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »