Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza Vifungashio kilichopo Wilayani
Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi, Katikati ni
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha na
kulia ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
akisalimiana na baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la
msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging
Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
akisaini kitabu cha wageni alipofika katika kiwanda cha kutengeneza
Vifungashio kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweka
Jiwe la Msingi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
(Katikati), Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph
Wasonga(kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC) Mlingi Mkucha wakielekea ndani ya kiwanda kuangalia mitambo na
hatua iliyofikiwa kabla ya kuanza kazi ya kiwanda hicho.
Mitambo itakayotumika katika kuzalishia vifungashio ikiwa tayari imekwisha fungwa tayari kwa kuanza kazi.
Mkurugenzi
Muendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging
Limited Bw. Joseph Wasonga na wafanyakazi wa kiwanda wakimtembeza
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
na kumpa maelekezo mbalimbali juu ya hatua iliyofikiwa kabla ya kiwanda
hicho hakijaanza kufanya kazi na kuzalisha vifungashio.
Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akiongea
wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza
vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha
Mkoani Pwani na kuwataka watanzania wenye nia ya kuwekeza katika sekta
ya viwanda kupeleka maandiko ya miradi yao katika shirika hilo na
watampa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kutimiza lengo la serikali ya
awamu ya tano ya kuwa na serikali ya viwanda.
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana akiongea wakati wa hafla ya
uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha
Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na
kumshukuru muwekezaji wa kiwanda hicho kwa kuamua kuwekeza katika mkoa
wa pwani kwani itaisaidia kuongeza mapato katika mkoa na kuongeza ajira
kwa wakazi.
Mkurugenzi
Muendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging
Limited Bw. Joseph Wasonga akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la
msingi katika kiwanda hicho na kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake
ikiwemo NDC, NEMC,TBS na Ofisi ya Mkoa wa Pwani kwa ushirkiano
walioupata wakati wa mchakato wa uanzishaji wa Kiwanda hicho hadi hapo
kilipofika na kuzitaka taasisi za fedha nchini kuendelea kutoa mikopo
yenye riba nafuu kwa ajili ya kuwaaidia wawekezaji wazawa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha
kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani
Kibaha Mkoani Pwani ambapo alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho na
kutoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuweka mazingira mazuri
kwa ajili ya wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya
viwanda kama ilivyo katika mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
(katikati)akikata utepe kuashirika uwekaji wa jiwe la msingi katika
kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging kilichopo
Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Muendeshaji
wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga, watatu kutoka kushoto ni Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akifuatiwa na
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
(katikati mwenye miwani), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC) Mlingi Mkucha (mwenye tai nyekundu), Mkurugenzi Muendeshaji wa
Kiwanda cha vifungashio Bw. Joseph Wasonga (wanne kutoka kulia) na Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Kiwanda hicho na wafanyakazi wa NDC.
PICHA HABARI NA HASSAN SILAYO
Wakuu
wa Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kuweka kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji nchini ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa
viwanda nchini.
Akizungumza
wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza
vifungashio kilichopo wilayani Kihaba mkoani Pwani Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa tukiwa
tunaelekea katika nchi ya viwanda serikali inajukumu la kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji nchini.
Dkt.
Adelhelm amesema kuwa viongozi hao hawana budi kuiga mfano wa Mkuu wa
Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano wanaoutoa kwa
wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika
mkoa huo.
“Dhumuni
la serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunaifikia nchi ya uchumi wa kati
kupitia viwanda,na hili tutalitekeleza pia kwa kushirikiana na sekta
binafsi na ni jukumu la viongozi ikiwemo wakuu wa wilaya na wakuu wa
mikoa nchini kote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji ikiwemo
kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda”. Alisema Dkt. Adelhelm.
Dkt.
Adelhelm aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2020 Serikali imepanga
kuhakikisha sekta ya viwanda nchini inachangia asilimia 15 kwenye pato
la taifa kutoka asilimia 7.3 iliyopo hivi sasa.
Pia
Dkt. Adelhelm alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya ajira za
viwandani na ajira zitokanazo na sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia
40 ifikapo mwaka 2020.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) Bw. Mlingi Mkucha
amesema kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji
wote wenye nia ya kuwekeza katika viwanda ikiwemo kupitia maandiko ya
miradi yao na kuwasimamia ili kuhakikisha kwa pamoja wanatimiza lengo la
serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Bw.
Mkucha aliongeza kuwa katika wilaya ya Kibaha kuna hekari 330
zilizotengwa kwa ajili ya viwanda vya aina mbalimbali ikiwamo viwanda
vya kuunganisha magari, vuwanda vya madawa na viwanda vya nguo hivyo
kama kuna muwekezaji mwenye nia ya kuwekeza katika sekta hizo aende
katika ofisi za Shirika hilo ili kuweza kujadili namna ya kutekeleza
suala hilo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana alisema kuwa ujenzi wa
kiwanda hicho katika mkoa wa pwani ni mwendelezo wa jitihada za kumuunga
mkono Rais Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza
vifungashio cha Global Packaging Bw. Joseph Wasonga alishukuru jitihada
za serikali na taasisi zake kwa ushirikiano wanaoupata tangu wakiwa na
wazo la kuanzisha kiwanda hicho hadi kufikia hatua hiyo ya uzinduzi.
Bw.
Wasonga aliongeza kuwa dhumuni la kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio
milioni 16 hadi milioni 20 kwa mwaka na kuongeza zaidi idadi ya ajira
kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka kiwanda hicho na maeneo ya jirani.
Kiwanda
cha hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la
Taifa(NDC) na kampuni ya Wande Printing and Packaging inayomilikiwa na
mzawa.
EmoticonEmoticon