NA DAUDI MANONGI, MAELEaZO.
Novemba
5 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John
Pombe Magufuli ametimiza mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani akiwa
na dhamira mpya ya serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mara
kadhaa Rais Magufuli amekuwa akisisitiza umuhimu wa viwanda ambapo
anasema vinaweza kutengeneza ajira kwa watanzania waliojiajiri wakiwemo
vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini.Katika
kutimiza azma iyo aliagiza mifuko ya Hifadhi ya Jamii ijikite zaidi
kwenye uwekezaji wa viwanda ili kuunga mkono lengo la Serikali.
Katika
kutekeleza agizo la Rais Magufuli tayari mfuko wa Pensheni wa PPF
umeanza kutekeleza agizo hilo kwa kuingia ubia na jeshi la Magereza na
kuanzisha kiwanda cha kuzalisha viatu na bidhaa za ngozi.Makubaliano
haya yalisainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio na Kamishna
Jenerali wa Magereza Bw.John Minja Octoba 4, 2016 katika ukumbi wa
mikutano wa makao Makuu ya Jeshi la Magereza uliopo Jijini Dar es
Salaam.
Aidha
katika makubaliano hayo PPF itakarabati na kuboresha miundombinu ya
kiwanda cha viatu cha karanga ambacho uzalishaji ulianza mwaka 1977 na
kufunguliwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pamoja
na kiwanda cha sasa PPF itajenga kiwanda kipya cha kisasa ambacho
kitakuwa kikisindika ngozi na kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi kwa
kutumia mashine za kisasa na teknolojia ya hali ya juu na hivyo kuongeza
uzalishaji na kupanua masoko ya viatu nchini na kuongeza pato la Taifa.
Akizungumza
wakati wa kutiwa saini mkataba wa makubaliano Mkurugenzi Mkuu wa PPF
Bw. William Erio alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ni utekelezaji wa
lengo la Serikali la kuwa na uchumi wa viwanda na faida kubwa kwa nchi
kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini kwa ajili ya soko la
ndani na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni ambazo zingetumika
kununua malighafi mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Vile
vile kiwanda hicho kipya kitatoa ajira kwa watanzania lakini pia PPF
itanufaika kwa faida itokanayo na uwekezaji pamoja na kupata wananchama
wapya watakaojiunga na mfuko huo.
Aidha
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uzalishaji katika kiwanda
kipya cha uchakataji ngozi unatarajiwa kuanza mwaka 2018 na kwamba
katika kipindi ambacho ujenzi wa kiwanda kipya utakuwa unaendelea kile
cha zamani kitaboreshwa ili kuongeza zaidi ufanisi wa uzalishaji.
Katika
hatua nyingine mfuko wa PPF umeanza hatua za awali za kuwekeza katika
kiwanda cha Sukari eneo la Mkulazi lililopo kilometa 195 kutoka Manispaa
ya Morogoro na km 75 kutoka Ubena-Zomozi barabara kuu ya Dar es Salaam
na Morogoro ambapo uwekezaji huo utafanyika kwa ubia kati ya PPF na NSSF
kwenye eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 63000 ambapo tayari kampuni
ya pamoja imeshaanzishwa azma hiyo.
Kiuchumi
eneo la Mkulazi liko karibu na Reli ya kati kwenye kituo cha Ngerengere
na lipo karibu na Reli ya TAZARA kupitia kituo cha kidunda hivyo
uwekezaji katika eneo hilo utafanya usafirishaji wa malighai na bidhaa
kuwa rahisi.
Kiwanda
hicho kitazalisha zaidi ya tani 200,000 za Sukari kwa mwaka lakini pia
kitatoa ajira za moja kwa moja na ajira shirikishi kwa watanzania zaidi
ya 100000 na hivyo kutimiza lengo la Rais na Serikali yake katika
kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira pamoja na kuongeza pato la Taifa.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF Bw.William Erio alisema uwekezaji huu utafanyika katika
awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha uzalishaji wa Miwa na
ujenzi wa kiwanda cha Sukari na awamu ya pili utahusisha kilimo cha
nafaka kama vile Mahindi,Mpunga na Mtama.
PPF
itaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kufanikisha azma
yake ya Tanzania ya viwanda kwa kuwekeza katika maeneo yenye tija kwa
mfuko ili kukuza uwekezaji na tija kwa wanachama na jamii kwa ujumla.
Katika
kuzidi kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano na falsafa yake ya “Hapa
kazi tu” PPF itafanya uwekezaji wa ujenzi wa jengo la kiwanda kwenye
kiwanda cha nguo cha Touku kilichopo eneo la Mabibo katika ukanda
maalumu wa kiuchumi wa Benjamin Mkapa ambapo kiwanda hiki huzalisha nguo
zenye ubora kwa ajiri ya soko la Marekani kupitia mpango wa ukuzaji
fursa za kiuchumi Afrika AGOA(African Growth and Opportunity Act uku
uwekezaji wa Jengo la kiwanda utapanua wigo wa ajira kwa watanzania
kutoka 1600 waliopo sasa mpaka kufikia ajira 7000.
Mfuko
wa PPF unaendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwafikia
watanzania wajasiriamali ili kuboresha biashara na maisha yao.
Sanjari
na hilo tayari PPF imeanzisha mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao
kama Wote Scheme ambao unawalenga wanachama waliojiajiri wenyewe katika
sekta isiyo rasmi ambao kwa mujibu wa takwimu za kitaifa sekta hiyo
inachukua zaidi ya asilimia 90 ya nguvu kazi ya Taifa.
Mfuko
huu unawalenga watu waliojiajiri katika makundi ama mtu mmoja wakiwemo
wakulima, wavuvi, wafugaji, madereva wa daladala, bodaboda
,mabasi,Teksi,Mama lishe,Wajasiriamali mbalimbali wenye maduka na
biashara nyingine pamoja na vikundi vya Vikoba.
Kwa
kupitia mfumo wa wote Scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata
bima ya afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni
ya uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.
Kupitia
mfumo wa wote scheme watanzania watakuwa na uhakika wa kupata bima ya
afya,mkopo wa elimu na maendeleo ya biashara pamoja na pensheni ya
uzeeni endapo mwanachama atafikia kiwango cha kustaafu.
Kupitia
mfumo wa wote scheme mwanachama anaweza kuchangia kiwango kisichopungua
elfu ishirini kwa mwezi au zaidi na mfumo huu ni rahisi sana ambapo
wanachama wanaweza kulipa michango yao kwa simu ya mkononi kupitia
mifumo kama vile M-pesa,Airtel Money,Tigo Pesa popote pale walipo eneo
lao la kazi bila hata kufika ofisi za PPF.
Pamoja
na hayo tunayaomba makundi mbalimbali ya wajasiriamali walioko katika
sekta isiyo rasmi kujiunga na mfumo huu kwa faida ya maisha yao ili
waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa katika mfumo huu.
Pamoja
na Mfuko wa PPF kusajili wanachama kukusanya michango kuwekeza na
kulipa mafao imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za
kijamii kama vile afya,elimu na kuchangia kwenye maendeleo ya jamii
katika kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kwenye
sekta ya elimu mfuko wa PPF umekuwa mstari wa mbele kuchangia
changamoto ya upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari
kitaifa.
PPF
imeendelea kuunga mkono mpango wa serikali katika kutatua changamoto ya
madawati kwenye shule mbalimbali ambapo mfuko umechangia shilingi
milioni 200 katika kufanikisha mpango huo uku lengo kuu la mfuko wa PPF
likiwa ni kuhakikisha wanafunzi hawasomi wakiwa wamekaa chini kwani ndio
nguvu kazi ya Taifa la Kesho na ni wanachama watarajiwa katika mifuko
ya hifadhi ya jamii ikiwemo PPF.
EmoticonEmoticon