Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akisikiliza kero za harufu kali za mabwawa ya maji taka kutoka kwa wana nchi yaliyopo Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada
ya kufanya ziara kukagua miundo mbinu ya Dawasco inayolalamikiwa na
wana nchi kwa kutiririsha maji machafu sehemu za makazi, jijini Dare
s salaam mapema hii leo.
EVELYN
MKOKOI
AFISA
HABARI
OFISI
YA MAKAMU WA RAIS
DAR
ES SALAAM
Katika hali isiyo ya kawaida shirika la
maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar Es Saaal na Pwani DAWASCO, limeingia mitini katika
Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya
kutembelea miondombinu ya maji taka na maji safi Jinini dar Es
Salaam na Pwani Leo.
Licha ya Shirika Hilo kupewa Taarifa ya Ziara ya Naibu waziri Mpina
mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa kumuwasilisha
mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.
Akiongea kwa ukali baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha maji taka
kwenda baharini la Ocean road, Naibu Waziri Mpina amesema ubovu wa bomba
la ocean road unatokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha
dhahiri kuwa DAWASCO wana Jeuri kwa IKulu, kwa kutokulifanyia ukarabati
kwa muda muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo hayo.
Alipotembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni, Mhe Mpina
Alisema pamoja na kuwa miondombinu hiyo inaelemewa na wingi wa
wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husina zina wajibu wa kuyafanyia usafi
mabwawa hayo lakini, hazijaonekana jitihada zozote za kufanya hivyo,
na miondombinu hiyo inaonekana kutofanyiwa ukarabati kwa muda wa miezi
sita.
Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa miundombinu
hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha ya
wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.
Akiongea kwa Uchungu, Mkazi mmoja wa Mabibo aliyekataa kutaja jina
lake alisema kuwa, ninanukuu“Mabwawa haya ni ya Dawasco na hata tukitaka
kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao kuelekea kwenye mabwawa wana
taka tuwalipe na tunafanya hivyo, wenye viwanda halikadhalika wanawalipa
dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu ya dawasco, lakini
najiuliza, kwa nini wanakuwa wagumu kuyafanyia ukarabati au hata kusafisha
tuu?. Mwisho wa kunukuu.
Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundiombinu ya DAWASCO leo
Jijini Dar Es Saalam ilihushisha maafisa kutoka DAWASA na BAraza la
taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi
yote inayosimamiwa na DAWASCO na kuon akama wanatenda haki katika kutoa
huduma kwa wananchi.
EmoticonEmoticon