Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh Luhaga Mpina akikagua mto kibangu ambao umechafuliwa
na maji yanayotiririshwa na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo tabata
jijini dare s salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati)akitembezwa ndani ya kiwanda
cha Urafiki Textile mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho
mapema hii leo
EVELYN MKOKI AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
DAR ES SALAAM
4/8/2016
Kiwanda cha kutengeneza
nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa
faini ya shilingi milioni Thelathini kwa kosa la uchafuzi w a mazingira
kwa kutiririsha maji taka na yenye sumu katika mto kibangu kuhatarisha
maisha ya mazingira na viumbe hai pamoja na kiwanda hicho kuwa
na mazingira machafu na hivyo kuatarisha maisha ya wafanyakazi kiwandani
hapo.
Faini hiyo inayotakiwa
kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi
waMazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya kukagua viwanda na
mazingira nchini ambapo sambamba na adhabu hiyo kiwanda hicho kimetakiwa
kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo, pamoja kupeleka
repoti ya upimaji wa moshi, vumbi litokanalo na makaa ya mawe na maji
yanayotoka kiwandani hapo ili serikali kujiridhisha kama si hatarishi
kwa mazingira.
‘’Ili kujiridhisha
NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji haya yanayotiririka ili tuone
kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na kiwanda kiwasilishe cheti
cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu Waziri Mpina.
Kwa upande wake Meneja
wa kiwanda hicho Bwana Mohamed Rajabu alipoulizwa kama ameikubali adhabu
hiyo, alitupia lawama kwa NEMC na kusema kuwa wao ndo walitoa kibali
cha athari ya tathimini ya mazingira kwa kiwanda hicho na ndiyo maana
kinaendelea kufanya kazi na kuwa wangekuwa wanapita kwanza na kutoa
onyo kwa wenye viwanda kabla ya kutoa adhabu kali ya mamilioni ya fedha,
na kuongeza kuwa kukabiliana na faini kubwa hivyo kwa kiwanda hicho
kunaweza kupelekea wafanyaki kupoteza ajira zao kwa kupunguzwa kazini.
Akiitimisha katika zoezi
hilo Naibu waziri Mpina aliwataka wawekezaji na wenye viwanda nchini
kutii sheria na kuthamini maisha ya wafanyakazi kwa kuyaweka mazingira
safi na salama.
EmoticonEmoticon