Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya
Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya
Dung’unyi katika Tarafa ya Ikungi
Kikosi cha vijana wa Mgambo
kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao
katika mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa
mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na
usalama ya Wilaya ya Ikungi
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka
Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi
kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus
Ndalama
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne
Mtaturua akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada
ya ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16
……………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida
Wiki 16, Miezi minne itatosha
kuwakutanisha pamoja vijana wa kata mbalimbali Wilayani Ikungi kwa
pamoja wakipatiwa mafunzo ya Mgambo hususani kujifunza uzalendo, Mbinu
za medani za kupambana na uhalifu, Kuimarisha nidhamu na kujituma.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti
wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji
Jumanne Mtaturu wakati akifungua rasmi mafunzo hayo yatakayojikita pia
katika kuimarisha utu na uadilifu.
Mtaturu amesema kuwa vijana wote
walioamua kujitolea katika mafunzo hayo kwa ridhaa yao watapaswa kuwekwa
katika kumbukumbu ya vijana ambao baada ya kumaliza mafunzo
wataanzishiwa vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitasimamiwa na Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya.
“Tanzania ina wimbi la vijana
wengi ambao wanajiamulia maisha wenyewe kutokana na wazazi wao
kuyakimbia majukumu yao ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ya
kumjua Mungu na nidhamu kwa kila mtu kwenye jamii hivyo sisi kama
serikali ngazi ya Wilaya tutahakikisha Vijana hawa wanaimarika katika
maadili mema” Alisema Mtaturu
Dc Mtaturu amesema kuwa mara baada
ya kumalizika kwa mafunzo hayo vijana hao watapaswa kuamua wanataka
kujishughulisha na nini kati ya ufugaji na kilimo cha kisasa ambapo
ofisi ya mkuu wa Wilaya itasimamia kuhakikisha wanafanikiwa katika
malengo yao.
Sambamba na hayo amewaeleza vijana
hao kuwa serikali ina mamlaka ya kuwasaidia watanzania kujikwamua
katika wimbi kubwa la umasikini lakini pia vijana na watanzania kwa
ujumla wanapaswa kutumia muda wao mwingi kujishughulisha na shughuli za
uzalishaji mali kwa kufanya kazi sio kucheza bao, kujihusisha na vikundi
ovu, kunywa pombe, Ngono zembe ama kucheza Pool Table wakati wa kazi.
Dc Mtaturu amewapongeza vijana hao
kwa kujitolea kwa moyo mmoja kushiriki katika mafunzo hayo ambapo
amesema kuwa mafunzo wanayoyapata sio mateso ila ni sehemu ya
kuwaimarisha kimwili na kiakili, Kujifunza maadili mema, ili kuwa na
uchungu na nchi yetu.
Mafunzo ya mgambo yaliyofunguliwa
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu yanahusisha Tarafa
mbili ya Ikungi na Sepuka ambapo katika Tarafa ya Ikungi vijana wa kiume
waliojitokeza ni 138 huku wanawake wakiwa 6.
Kwa upande wa Tarafa ya Sepuka kuna jumla ya vijana 210 ambapo vijana wa kiume ni 206 na wanawake ni wa 4.
Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo
katika Tarafa hizo mbili Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi aliambatana na
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya.
Dc Mtaturu amesisitiza kuwa mgambo
wanajulikana kama jeshi la akiba ambapo wajibu wao Mkubwa ni
kushirikiana na jeshi la polisi na Jamii katika kuimarisha ulinzi wa
watu na Mali zao.
EmoticonEmoticon