Profesa Muhongo aelezea mikakati Sekta za Nishati na Madini, Benki ya Dunia yafurahishwa na utekelezaji wake

June 14, 2016

mug1 
Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo  akiongoza kikao kilichoshirikisha Watendaji kutoka  Benki ya Dunia pamoja  na watendaji kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini na   taasisi zake ikiwa ni pamoja na  Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA).
mug2 
Mtendaji  Kutoka Benki ya  Dunia anayeshughulikia mazingira  Vladislav Vucetic, akielezea mikakati ya   benki hiyo katika ushirikiano wake  na  Serikali ili  kupanua sekta za nishati na madini.
mug3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa  Justin Ntalikwa (kushoto waliokaa mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati Dkt. Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka  kushoto waliokaa mbele) wakifuatilia kwa makini maelekezo 
…………………………………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameelezea mikakati ya   Serikali katika  uboreshaji wa sekta za nishati  na  madini  na kuongeza kuwa  Serikali ipo  tayari kushirikiana na    Benki ya Dunia (WB) katika uboreshaji  wa sekta hizo ili ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo alipokutana na Watendaji kutoka  Benki ya Dunia pamoja  na watendaji kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini na   taasisi zake ikiwa ni pamoja na  Shirika la  Umeme  Tanzania (TANESCO), Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na Wakala wa Serikali  wa Uagizaji wa Mafuta ya Pamoja (PBPA)
Akizungumzia Sekta ya Nishati  nchini Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa  Sekta ya nishati inakuwa na mchngo mkubwa katika ukuaji wa uchumi  na kutoka katika kundi la nchi masikini duniani  na kuingia katika kundi la nchi  zenye kipato cha kati ifikapo mwaka  2025 kama Dira ya Maendeleo  ya Taifa ifanvyofafanua
Aliongeza kuwa, Serikali kwa mara ya kwanza imetenga  asilimia  40 ya bajeti yake katika miradi ya  maendeleo  ikiwa ni  pamoja na ya  umeme na kuendelea kufafanua kuwa katika bajeti  ya  Wizara ya  mwaka wa  fedha  2016/17, Wizara imetenga asilimia 94 ya bajeti yake katika miradi ya maendeleo,  ambapo  katika Idara ya Nishati asilimia 98 itakwenda kwenye miradi ya umeme.
Waziri Muhongo alisema  kuwa ili kuimarisha   Sekta ya Nishati,  Wizara imepanga kupanua sekta ya nishati kwa kukaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza  katika sekta ya uzalishaji na uuzaji wa umeme pamoja na kuwapo kwa mwongozo utakaowawezesha kuzalisha umeme.
Alindelea kusema kuwa Wizara inatarajia kuimarisha  usambazaji wa umeme vijijini kwa kushirikiana na  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na TANESCO.
Profesa Muhongo aliendelea kutaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na  kuimarisha mradi wa usambazaji wa umeme  wenye msongo wa kilovolti  400 kupitia  Iringa, Mbeya, Tunduma hadi katika eneo la Kabwe nchini  Zambia  na  kusisitiza kuwa upembuzi  yakinifu unatarajia kukamilika mapema  Desemba mwaka huu kabla ya kuanza kwa mradi.
Aliendelea kutaja miradi mingine kuwa ni pamoja na mradi wa usambazaji  umeme kupitia Mbeya, Sumbawanga, Mpanda, Kigoma, Nyakanazi na kuiomba  Benki ya Dunia kushirikiana na Benki ya Maendeleo  Afrika (AfDB) ili kufanikisha mradi huo.
“Kuna mradi wa kuunganisha  Tanzania  na  Uganda ujulikanao kwa  jila la  Tanzania – Uganda inter-connector unaounganisha Mwanza, Geita,  Nyakanazi, Kyaka- Bukoba hadi  Masaka nchini Uganda.
Akizungumzia  Sekta ya  Gesi  Profesa Muhongo  alieleza kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha nishati ya  gesi inatumika  ipasavyo katika uzalishaji  umeme pamoja na kusambazwa katika matumizi ya majumbani.
Aliongeza kuwa serikali imeweka mikakati ya kusambaza gesi majumbani kwa ajili ya matumizi ya kupikia katika mikoa ya Dar es salaam, Lindi, Mtwara na katika maeneo mengine ya  Pwani.
Akielezea Sekta ya Madini  Profesa Muhongo aliiomba Benki ya  Dunia kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya madini kwa wachimbaji wadogo pamoja na katika kuwapatia  elimu  kuhusu mazingira, uchenjuaji wa madini  na kuongeza ajira  hususan katika maeneo  ya madini yaliyopo  vijijini
Naye Mtendaji  Kutoka Benki ya  Dunia anayeshughulikia mazingira  Vladislav Vucetic alisema  Benki ya Dunia ipo   tayari kushirikiana na Serikali katika uendelezaji wa sekta za nishati na madini ili kufikia malengo  yaliyokusudiwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »