KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NGAZI ZA JUU MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA

June 14, 2016

KT1 
Gwaride la Maafisa Wahitimu wa kozi ya Uongozi ngazi ya Juu wa Jeshi la Magereza likijiandaa kupita mbele ya Jukwaa la Mgeni kwa heshima kama wanavyoonekana wakiwa wakakamavu katika picha. Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zimefanyika leo Juni 14, 2016 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.
KT2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua Gwaride la Wahitimu kama inavyoonekana katika picha.
KT3 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akimvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu aliyefanya vizuri katika masomo ya Medani kwa niaba ya Wahitimu wote wa kozi hiyo(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akishuhudia tukio hilo la uvishaji cheo.
KT4 
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wageni Waalikwa kutoka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa karibu Gwaride la Wahitimu.
KT5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi juu ya Uendeshaji wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani).
KT6 
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kulia) akimuongoza Mgeni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira kuelekea eneo la hafla ya kufunga rasmi Mafunzo ya Uongozi ngazi za juu wa Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, ACP. Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »