Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amempongeza Ravia Idarous Faina wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha
Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika
ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba.
Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa
kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA
katika kipindi kingine.
Malinzi amewapongeza vingozi wote wapya waliochaguliwa katika
uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli zote
za maendeleo ya mpira wa miguu.
Uchaguzi wa kupata viongozi wa ZFA ulifanyika jana Gombani kisiwani
Pemba, ambapo Ravia aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake, nafasi ya
makamu wa rais Ugunja kienda kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba
ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.