Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea wikiendi
hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku
kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika
mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC wakiwakaribisha
wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona mjini
Mtwara.
Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa
Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto
Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.