Naibu waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo atoa pongezi kwa Twiga Stars.

February 12, 2016

an1
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati) akipokelewa na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) alipofanya ziara katika katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an2
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wapili kulia) moja ya ofisi zinazotumiwa na TFF wakati Mhe. Waziri alipofanya ziara katika katika ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an3
Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine (aliyesimama) akizungumza na ugeni ulioongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutembelea ofisi za TFF pamoja na kuzungumza na wachezaji wa Twiga Stars leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge
an4
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Twiga Stars (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea ofisi za TFF na kukutana na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine
an5
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Twiga Stars leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara katika ofisi za TFF na kuzungumza na wachezaji hao kuwahamasisha wazidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine na wanne kulia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wanawake Bibi. Amina Karuma
an6
Wafanyakazi wa TFF katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (wanne kushoto) alipotembelea ofisi za TFF leo jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw. Makoye Nkenyenge na wapili kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
…………………………………………………………………………………………………………..
Na: Shamimu Nyaki – Maelezo
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars) kwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali wanayoshiriki ndani na nje ya nchi iliyopelekea kushika nafasi ya nane katika bara la Afrika kwa mwaka 2015.
Pongezi hizo amezitoa leo jijjini Dar es Salaam wakati alipozungumza na wachezaji hao  katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambapo wameweka kambi kwa ajili ya kujianda na Mchezo wao dhidi ya Zimbabwe utakaochezwa  mwezi  wa tano mwaka huu.
Mhe. Wambura amewataka  wachezaji hao kujituma kwa bidii, kuwa na nidhamu pamoja na kuzingatia maadili ya nchi yetu kwa kuwa wao ni mwanga wa jamii ili waweze kufika mbali kama mchezaji Mbwana Samatta.
“Mnapokuwa kambini zingatieni maadili, kanuni, sheria zilizopo na kuamini michezo ni ajira kwenu na inaweza kubadili maisha yenu kwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya uwezeshaji” Alisema Mhe. Wambura.
Aidha Katibu Mkuu wa Shrikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Bw. Mwesigwa Celestine akitoa taarifa fupi ya  utendaji wa Shirikisho hilo amesema kuwa kwa upande wa wanawake TFF inafanya juhudi  za kuanzisha ligi ya Taifa ya mpira wa Wanawake kutoa mafunzo kwa makocha wa mpira wa wanawake pamoja na kufuatilia vipaji vya watoto wa kike waliopo mashuleni.
Bw. Celestine ameeleza changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya shirikisho hilo ikiwemo baadhi ya sheria na kanuni zinazosimamia masuala ya mpira wa miguu Tanzania na FIFA zimekuwa zikitofautiana na sheria za nchi kwa kuwa hazijafanyiwa marekebisho ili ziweze kua na uwiano ambapo Mhe. Naibu Waziri ameahidi kuzishughulikia.
Kwa upande wake kapteni wa Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) Bibi. Sophia Mwasikile amemshukuru Naibu Waziri kwa pongezi alizowapa na kuahidi kuwa wataendelea kufanya vizuri zaidi na kuitangaza nchi vizuri kupitia mchezo huo na kushika nafasi ya juu zaidi ndani na nje ya Afrika.
Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake Twiga Stars imekuwa ni timu pekee Tanzania inayofanya vizuri katika michuano inayoshiriki japokuwa haina wadhamini hivyo ni wakati wa wadhamini kujitokeza kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri zaidi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »