: Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akikabidhiwa zawadi kutoka
TBL kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto)
kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Lager alipomtembelea ofisini kwake leo
jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group
Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka kulia) na Meneja Masuala ya Nje na
Mawasiliano Bibi. Emma Oriyo
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini kwake leo
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akielezea jambo
alipotembelewa na Uongozi wa TBL na Excutive Solution ambao ni wadhamini
na waratibu wa Mbio za Kilimanjaro Marthon leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin na kushoto
ni Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirikiano Bibi. Georgia Mutagahywa.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin alipomtembelea ofisini
kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa
Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka
kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (MB) akimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin (kushoto) alipomtembelea
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa
Excutive Solution na Mshauri wa Mahusiano wa TBL Bw. Aggrey Marealle NA
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Bibi. Kushilla Thomas (wapili kutoka
kulia).
………………………………………………………………………………………………………
Na: Frank Shija, WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe 28
Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Hayo yamebainisha na Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio waratibu wa mbio hizo
Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es
Salaam.
“Mbio za Kili Marathon
zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya Chuo Kikuu
cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.
Marealle alisema kuwa Mbio hizo
zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo
marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya
Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21 zinazodhaminiwa na
Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu wanaotumia Baiskeli
za matairi matatu na Viti vya matairi zinazodhaminiwa na kampuni ya
mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa
na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt
Aliongeza katika mbio hizo
washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza kwa
mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya
shilingi milioni nne kila mmoja.
Aidha alisema kuwa zaidi ya
washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati yao takribani
washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.
Kilimanjaro Marathon inatimiza
miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa mashindano hayo ni
Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na Executive
Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya
Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.