Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara
nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta
binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi
katika kupata huduma za jamii.
Naibu
Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano
wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali
inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili
kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
Makamu
Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa
mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na
wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi
katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika
kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika
mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali
inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili
kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Baadhi
ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini
jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi
katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika
kupata huduma za jamii.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali
imesema dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa
kupitia maeneo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti
ijayo ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana
nchini ikiwemo mzao ya misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia
wananchi.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa
akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam.
Dkt.
Mpango aliyaeleza maeneo hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa
katika bajeti hiyo ni pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa
na kutafuta wabia ambao wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.
Maeneo
mengine ni miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi
ili kuweza kupata matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas
kuwa yapo maeneo maalum ya kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na
Mtwara kutokana na maliasili iliyopo hapo.
Zaidi
ya hayo, Dkt. Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa
kutumia malighafi inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na
Mchuchuma itakuwa ni msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi
usiohitaji chuma”.
Katika
suala la ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango
alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya
usafirishaji ndani na nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mataifa mengine.
Mafanikio
ya ujenzi wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali
imedhamiria kushirikiana na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda
yanapaswa kuendana na maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu
inayoendana na mahitaji ya viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora
zaidi.
Aidha,
ili kujenga uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga
kukusanya kodi ambayo ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia
nchi kujiendesha ambapo wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili
na kupewa namba ya usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima
kupitia ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Katika
mkutana huo, Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za
biashara yao ili kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na
kuhimiza wafanyabiashara wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee
kuzitumia wanapouza bidhaa zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale
wasio na mashine hizo, Serikali inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la
kuwapatia mashine hizo.
Vile
vile, Dkt. Mpango ametoa namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha
Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja
kwa moja na Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa
mamlaka hiyo nchi nzima kwa namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa
namba 0689122516.
Aidha,
Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache
kufanyabiashara za magendo ambapo ameainisha baadhi ya maeneo
yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni,
ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.
EmoticonEmoticon