Mh:Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya
Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua
hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji
uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga
wilayani Mvomero.
Mh.Mwigulu
Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero
wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya
wakulima na wafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa
usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika
Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016
kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji
ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati
huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza
kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si
vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali
imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika
sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu
zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya
kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.
Mh:Mwigulu
Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa
wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo
la Mvomero.
Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.
Mwigulu
Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na
wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.
Mwigulu
Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake
kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji
cha Dihinda.
Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.
Mwigulu
akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara
yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la
kata ya Hembeti.
Waziri
wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya
Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa
wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya
wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.
Picha na Sanga Festo Jr.
EmoticonEmoticon