Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Serikali kushirikiana na Benki ya
Dunia inategemea kuanza ukarabati wa Miundo Mbinu mibovu hususani ya
mitaro inayosababisha maafa wilayani Temeke kuanzia mwezi Mei mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wilaya ya Tem
eke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.
eke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.
Hili limetokea baada ya uchunguzi
uliofanyika jana ambapo Mhandisi wa Wilaya, Bwana Afya pamoja na Afisa
Habari wa Wilaya walifika eneo la tukio na kuona hali halisi.
‘’Ni kweli maafa hayo yametokea
na sababu hasa ni miundo mbinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika
maeneo ya makazi ya watu,kwahiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi
yanapostahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu’’Alisema
Msumba.
Aliongeza kuwa ukarabati huo wa
mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es salaam Metropolitan Development
Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Aidha, Joyce Msumba amesema kuwa
endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza watatumia njia ya
kuyanyonya maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa
yasiendelee kutokea.
Mradi huu unalenga kuhamisha njia
za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi
ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende moja kwa moja baharin
EmoticonEmoticon