Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akizungumza leo katika
uzinduzi wa Kituo cha Damu salama kilichopo Mbagara Rangitatu jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akikata utepe kuzindua kituo cha
uchangiaji Damu salama cha Mbagala langitatu jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakijitolea damu katika kituo cha Rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
MPANGO
wa Taifa wa damu salama nchini ulio chini ya wizara ya afya maendeleo
ya jamii jinsia, wazee na watoto leo wamezindua kituo kidogo cha
uchangiaji damu kilichopo Mbagala Rangi tatu. Uzinduzi huu unaambatana
na uzinduzi wa vituo vingine vya afya vilivyopo wilaya zote za mkoa wa
Dar es salaam kama vile Amana, Mwananyama, Sinza, Vijibweni na Mbweni.
Viituo
hivi vimejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambao ni Hospitali
ya CCBRT, Hospital ya Mbweni Mission MDH, Umoja wa wamiliki hospital
binafsi (APHTA) NA Halmashauri za temeke Ilala na Kindondoni. Vilevile
Mpango wa Taifa wa Damu salama unawapongeza wachangia damu kwa hiari
ambao wamekuwa wakichangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya
wahitaji tangu kampeni hii ilipoa nza rasmi tarehe 3 februari 2016.
Maisha
ya watu wengi yanaokolewa kila mwaka nchini kwa kuongezewa damu .
Nchini Tanzania kinamama wengi na watoto hupoteza maisha kwa kukosa
damu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa nchini Tanzania
takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000 hufa kila mwaka
kutokana na uzazi na asilimia 80 ya hivyo vifo husababishwa na ukosefu
wa damu. Hivyo ufunguzi wa vituo hivi utasaidia kuondoa tatizo la uhaba
wa damu na hatimaye kutokomeza tatizo la vifo vinavyotokana na kukosa
damu.
Katika
mkoa wa Dare s Salaam mahitaji ya damu ni makubwa , kwa mwezi
tunahitaji chupa 4000 lakini zinazopatikana ni chupa 2000 tu ambayo ni
nusu ya mahitaji. Kuna wakati mahitaji haya yanakuwa makubwa zaidi na
hivyo upungufu huongezeka kufikia asilimia 70, hali ambayo ni hatari kwa
maisha ya binadamu.
Damu
ni uhai na haipatikani kwa njia yeyote ile isipokuwa kwa kuchangiwa na
binadamu wenzetu . Uchangiaji damu ni zoezi endelevu na la kudumu
kwakuwa damu huhifadhiwa kwa muda wa siku 35 tu tangu inatolewa .
Kutokana na uhifadhi wa damu kuwa ni wa muda mfupi ndio maana
inasisitizwa umuhimu wa watu kuchangia damu walau mara mbili kwa mwaka.