Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), alipokutana nao kabla ya kuongea na
Wafanyakazi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye koti la kaki), akisisitiza
jambo kwa Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL),alipokutana
nao jijini Dar es Salaam.
Rubani Lilla Borri wa Shirika la
Ndege la Tanzania (ATCL), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa
Wafanyakazi wa Shirika hilo na Waziri Prof. Mbarawa, uliofanyika katika
ofisi za Shirika hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiagana na Wafanyakazi wa Shirika
la Ndege Tanzania (ATCL), mara baada ya kuongea nao Ofisini Hapo.
Moja ya Ndege iliyokuwa ikimilikiwa na Shirika la Ndege la Air Tanzania
……………………………………………………………………………………………………………
Serikali imezungumzia umuhimu wa
kulifufua upya Shirika la Ndege nchini Air Tanzania (ATC) kwa
kulinunulia ndege mpya na kulipa mtaji ili lifanye kazi kibiashara na
kutengeneza faida kama ilivyokusudiwa awali.
gumza na menejimenti na wafanyakazi wa Shirika hilo alipolitembelea jijini Dar es Salaam leo.
“Tutawekeza kwenye Air Tanzania
ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuvutia wasafiri wengi kufika nchini
moja kwa moja na kuvutia sekta ya utalii”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amewataka
wafanyakazi wa Shirika hilo ambao sio waadilifu na wavivu kuondoka mara
moja ili kupisha wafanyakazi wabunifu na wenye mawazo ya kibiashara
kuendesha shirika hilo kwa faida.
“Tunataka watu watakaolitoa
shirika hili kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuliwezesha kiuchumi
na kujitegemea ili kushindana na mashirika mengine ya ndege katika
biashara“, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli yuko tayari
kununua ndege mpya ili kulifufua shirika hili hivyo amewataka
wafanyakazi hao kuwa na mtazamo chanya wa kufanya biashara ili kuiletea
taifa tija.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa ATC Bw. Johnson Mfinanga amemwambia Waziri Prof. Mbarawa kuwa
kwa sasa shirika hilo lipo katika hali mbaya kiuchumi na hivyo kuhitaji
nguvu ya Serikali kulikwamua ili litoe huduma inayoshahili.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa
amesisitiza kuwa Serikali itaangalia upya taratibu za ajira katika
shirika hilo na watakaobainika kuajiriwa kinyume cha taratibu
watafukuzwa kazi mara moja.
“Tutanataka watu waadilifu,
wabunifu na wenye sifa stahiki ili wafanye kazi kwa maslahi ya shirika
na taifa kwa ujumla”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Shirika la Ndege nchini ATC toka
mwaka 2009 limekuwa likijiendesha kwa hasara na Serikali ya Awamu ya
Tano imedhamiria kulifufua shirika hilo ili lifanye kazi kwa faida na
kuboresha usafiri wa anga ndani na nje ya nchi na hivyo kuvutia wasafiri
wengi kuja nchini moja kwa moja.