Ligi Daraja la
Kwanza nchini (FDL) raundi ya 13 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa
timu 24 [kucheza michezo 12 katika viwanja tofauti, huku kundi A na C
kukiwa na ushindani mkali kwa kila timu kuwania kupanda ligi kuu ya
Vodacom msimu ujao.
Kundi A, African Lyon watawakaribisha Polisi Dar katika uwanja wa
Mabatini – Mlandizi, Ashanti United dhidi ya KMC uwanja wa Karume, huku
Jumapili Kiluvya wakiwakaribisha Polisi Dodoma uwanja wa Mabatini –
Mlandizi na Friends Rangers wakicheza na Mji Mkuu uwanja wa Karume
jijini Dar es salaam.
Kesho Jumamosi, Kundi B Polisi Morogoro watacheza dhidi ya Njombe Mji
uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Kurugenzi FC dhidi ya JKT Mlale uwanja wa
Wambi – Iringa, Burkinafaso dhidi ya Lipuli na Kimondo watawakaribisha
Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Vwawa – Mbozi.
Kundi C, Polisi Mara FC watawakaribisha Panone FC uwanja wa Karume
mjini Musoma, Geita Gold watacheza dhidi ya JKT Oljoro uwanja wa
Nyankumbu mjini Geita, JKT Kanembwa watakua wenyeji wa JKT Oljoro uwanja
wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, huku Rhino Rangers wakicheza dhidi ya
Mbao FC uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mjini Tabora.