Raundi ya saba ya Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) inaendelea
wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa nchini, kwa timu 24 kusaka pointi
kutoka makundi ya A,B,C na D kuwania nafasi nne za juu ili kuweza
kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Kundi A, Leo Ijumaa Abajalo Tabora watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja
wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, Green Warriors dhidi ya Singida United
uwanja wa Mabatin Mlandizi (jumatatu) na Mirambo FC watacheza dhidi ya
Transit Camp siku ya jumatatu uwanja wa Ali Hassani Mwinyi mkoani
Tabora.
Kundi B, Kesho Jumamosi AFC ya Arusha watakua wenyeji wa Alliance
Schools uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Madini FC watacheza dhidi ya JKT
Rwamkoma uwanja wa Mbulu, huku Bulyanhulu FC watawakaribsiha Pamba FC
uwanja wa Kamabrage mjini Shinyanga.
Kundi C, Leo Ijumaa Abajalo Dar watacheza dhidi ya Mshikamano uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam, kesho Jumamosi Kariakoo FC
watawakaribisha Changanyikeni katika uwanja wa Ilulu – Lindi, na
Cosmopolitani watacheza dhidi ya Villa Squad siku ya jumatatu katika
uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kundi D, Jumamosi Mighty Elephant watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja
wa Majimaji mjini Songea, Mbeya Warriors watawakaribisha Mkamba Rangers
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Jumapili Sabasaba FC wakicheza
dhidi ya African Wanderers uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.