Shillingi
Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General
Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa
Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya
kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya
utengenezaji wa matairi duniani.
Akijibu
swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA)
lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General
Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa
Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles
John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na
wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi
nchini.
“Tumeanzisha
viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio
kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza
kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu
tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya
kazi mara moja”
“Sio
tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda
vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda
hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji
wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.
Aidha
Mhe. Charles John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi
yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha
mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania
Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na
Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu
ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini
iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza
mikataba ya mauziano kikamilifu.
Ameongeza
kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili
tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili
kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John
Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya
taifa.
Serikali
kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali
itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli
zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya
kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha
Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na
ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo
la ajira nchini.
Imeandaliwa na Raymond Mushumbusi – MAELEZO