Mchezaji wa zamani wa timu ya
Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa
makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwasili katika Jengo la Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo leo. Kanu atakiwepo
nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na
kijamii.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Moyo, Dk Peter Kisenge katika taasisi hiyo akimkaribisha Nwankwo Kanu
Ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu
atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za
kampuni na kijamii.
Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi
wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akimsikiliza Daktari bingwa
katika Taasiai ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dk Peter Kisenge wakati akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu
ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akifafanua jambo kwa madaktari wa
taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya taifa ya
Muhimbili wakati alipotembelea hapo.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu
ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akimsikiliza mmoja wa madaktari wakati
alipotembelea katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo huku madaktari wa hospitali hiyo
wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mmoja wa wagonjwa katika Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili mtoto
Mariam Omary akifurahi baada ya kupata fursa ya kutembelewa na kujuliwa
hali na aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa
ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika.
Fatuma Shaban akipokea zawadi
kutoka kwa aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria na kwa
sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kwa
niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo
kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya
Taifa ya Muhimbili.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu
ya Taifa ya Nigeria Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika akizungumza jambo na madaktari katika chumba
cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) alipotembelea taasisi
ya moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
……………………………………………………………………………………………………………………..
Aliyekuwa mchezaji nguli wa timu
ya taifa ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia kwa sasa ni
balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika leo ametembelea Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) kwa lengo la kujua ni jinsi gani taasisi hiyo inafanya
kazi pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa moyo waliolazwa katika Taasisi
hiyo. pia
Akizungumza baada ya kuwasili
katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo
hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuahidi kubadilishana
uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi
hiyo.
“Tatizo la moyo ni kubwa sana kwa
sasa na limekuwa likiongezeka kwa kasi lakini cha kusikitisha ni kuwa
sio kila mtu anaweza kumudu gharama za matibabu yake. Hivyo basi kuna
umuhimu mkubwa sana kwa serikali na wadau wengine kuanzisha vituo
maalumu kama hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.” Alisema Kanu
Katika mazungumzo yake mchezaji
huyo wa nyota wa zamani ambaye aliwahi kuwika na vilabu kama vile vya
Arsenal, Ajax na Inter Milan, amesema kuwa pamoja na kuja kwa shughuli
mbalimbali kama balozi wa kampuni ya StarTimes lakini pia ana nia ya
kushirikiana na watalaamu wa Taasisi hiyo ya Moyo. Alielezea kuwa lengo
ni kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao
hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.
“Nimefarijika sana kuona serikali
ya watu wa Tanzania inachukua hatua stahiki katika kuwasaidia wananchi
wake. Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watanzania hasa
wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani
ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona. Tumeona mifano
michache ya wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika na kwingineko
duniani wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya mchezo kutokana
na kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha balozi huyo wa
StarTimes barani Afrika
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa
Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt.
Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai mwaka jana mpaka sasa tasisi
hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi wamewafanyia
upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo Kanu mbali na kujizolea
umaarufu na heshima kubwa katika medani za soka barani Afrika na Ulaya
yeye pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo alipoamua
kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu Heart Foundation.”
Taasisi yake hiyo iliyoko nchini
Nigeria ambako ndiko alipozaliwa aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya
kusaidia wenye matatizo kama yake na ameahidi taasisi hiyo kushirikiana
na taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika masuala mbalimbali.