Makamu wa pili wa Raisi Balozi
Seif Ali Iddi akipokea salamu ya heshima kwa Maafisa na wahitimu wa
mafunzo ya uongozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
Makamu wa pili wa Raisi Balozi
Seif Ali Iddi akikagua kwaride rasmin aliloandaliwa na Jeshi la Polisi
alipofika kufunga mafunzo ya ungozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani
Zanzibar.
Makamu wa pili wa Raisi Balozi
Seif Ali Iddi akimvisha cheo mmoja waaskari waliofanya vizuri zaidi
G.944 Makuza Azekiel Shuka kwa niaba ya wenzake katika sherehe ya
kumaliza mafunzo ya uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu
Sajenti yaliyofanyika Chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
Maafisa na wahitimu wa uongozi
mdogo wa Jeshi la Polisi wakitoa saluti kwa mgeni rasmini Makamu wa pili
wa Raisi Balozi Seif Ali.
Makamu wa pili wa Raisi Balozi
Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi
la Polisi katika viwanja vya Jeshi hilo Ziwani Zanzibar. Picha zote na
Makame Mshenga-Habari Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Khadija Khamis /Maryam Kidiko –Maelezo Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wahitimu wa mafunzo ya uongozi
mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mageuzi makubwa ya
utendaji katika sehemu zao za kazi.
Balozi Seif ameeleza hayo leo
katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi ngazi ya
koplo, sajenti na staff sajenti yaliyofanyika katika viwanja nya Polisi
Ziwani mjini Zanzibar.
Amesema kuyatumia mafunzo hayo
vizuri katika utendaji wa kazi itapelekea kupunguza uhalifu na
kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea mtabadilika na kuwa
watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka , haki
itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binaadam zitazingatiwa
kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu
baina yenu na Wananchi “Alisema Balozi.
Aidha alilitaka Jeshi la polisi
kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimae hupelekea
uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.
Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar
Hamdani Omar Makame amewakumbusha wahitimu hao kuwa wanawajibu mkubwa wa
kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.
Hata hivyo amewataka kufanya kazi
kwa kutumia elimu waliyoipata chuoni kwa vitendo, kuwaelimisha na
kuwaongoza kwa uweledi askari huko vituoni mwao.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa
chuo cha Polisi Zanzibar Deusdedit Kaizilege Nsimeki amesema Jeshi la
polisi litaendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi ili kuwajengea
uwezo na uwelewa wa umuhimu wa utii wa sheria bila ya kushurutishwa.
Mafunzo ya uongozi mdogo wa vyeo
vya Koplo, Sajenti na Staff sajenti yalifunguliwa rasmi tarehe
16/02/2016. Yakiwa na jumla ya wanafunzi 1532 kati ya hao kozi ya koplo
591, kozi ya Sajenti 706 na kozi ya Staff sajenti 235.