Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bw.
Jowika Kasunga akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina (kushoto) wa namna ambavyo
wilaya imeelekeza Kiwanda cha Mbao cha Sao Hill na Green Resources
Limited cha Mufindi kutunza Mazingira, (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Kiwanda hicho Bi Roselyne Mariki.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia kipande cha gogo ambacho ni moja ya waste product
(taka) inayotoka katika kiwanda cha Sao Hill and Green Resources
Limited baada ya uzalishaji wa mbao na nguzo ambayo taka hiyo ya gogo
pia hutumika kutengenezea gundi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitoa maelekezo kwa uongozi wa
kiwanda cha Sao Hill and Green Resources Limited, wa namna ya kuondosha
taka za nguzo (hazipo pichani) zilizozagaaa katika eneo la kiwanda
hicho..alipofanya ziara ya viwanda, ukaguzi wa usafi wa mazingira na
kupanda miti Mkoani Iringa leo.(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya
Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………………..
Kiwanda cha kuzalisha karatasi
cha Mufindi Paper Mills kilichopo wilayani Mufindi Mkoani Iringa,
kimetozwa faini ya shilingi milioni ishirini kwa kukiuka sheria ya
usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.
Faini hiyo inayotakiwa kulipwa
katika kipindi kisichozidi wala kupungua wiki mbili imetokana na
ukiukwaji wa sheria ya mazingira kwa utiririshaji wa kemikali hatarishi
kwa viumbe hai na mazingira katika mto kigogo, na maeneo ya jirani na
vijiji vinavyo uzunguka mto huo.
Akimfafanulia Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina alipofanya
ziara kiwandani hapo, Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) kanda ya Nyanda za Juu kusini. Bw. Godlove
Mwaisojo, ameeleza kuwa moshi, vumbi na majitaka yanayotoka katika
mitambo ya kiwanda hicho baada ya uzalishaji wa karatasi, yamezidi
viwango vya sheria kwa kuwa na kemikali hatarishi kwa baiyonuwahi na
mazingira na hivyo Baraza limekuwa likielekza mara kadhaa uongozi wa
kiwnda hicho kurebisha mfumo wa utoaji taka bila utekelezaji wa aina
yoyote.
Bw. Mwamsojo alimueleza Mh Naibu
Waziri Mpina Kuwa, kiwanda hicho kimeshauriwa na baraza kuhakiki ubora
wa hali wa hewa, na mitambo yao ya uzalishaji lakini kilikaidi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mufindi Bw. Jowika Kasunga, amemueleza Mh. Naibu Waziri Mpina kuwa,
pamoja na ukiukwaji wa utekelezaji wa sheria ya mazingira unaofanywa na
kiwanda hicho, pia menejimenti ya kiwanda hicho imekuwa na mgogoro
mkubwa wa ardhi na mahusiano mabaya na wanakijiji wanaozunguka kiwanda
hicho, na kuwa karibia hekta elfu kumi na nne za misitu zilizopo
katika eneo hilo, zipo katika mgogoro wa muda mrefu baina ya wanakijiji
na muwekezaji huyo, ambapo mgogoro huo umepelekea eneo hilo kutotumika
na wanakijiji wala muwekezaji huyo.
Mh. Naibu Waziri Mpina, ameutaka
uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wizara husika kutatua
mgogoro huo wa ardhi, ili uzalishaji wa rasilimali ya misitu uendelee
kwa manufaa ya taifa.
Kwa upande wake Mkuregenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Bw. CHOUDARY
kutoka barani Asia, alikubaliana na adhabu hiyo na kuhaidi kurekebisha
mitambo ya uzalishaji katika kiwanda hicho kwa kipindi kisichozidi wiki
mbili.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina, pia
ilihusisha ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha uzalishaji mbao,nguzo
na nishati cha Sao Hill and Green Resources Limited, cha Mjini Mufindi
na kujionea namna ambavyo kiwanda hicho kinavyokabiliana na athari
zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kwa kumiliki mashamba makubwa ya
misitu katika vijiji vya Mapanda na Achimbile, na kufanya biashara ya
hewa ukaa.