Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka
Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati
alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za
ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha
Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu
Salum .
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati)
Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa
za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi
Picha Na raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO
Dar es Salaam
Jumla ya shilingi trilioni 1.4
imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi
Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kiasi hicho ni sawa na ongezeko
la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani
wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo ,TRA ilikuwa
imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.
Takwimu hizo zimetolewa leo
jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa
taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.
Ameongeza kuwa katika kipindi
cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa
imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na
asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.
Kaimu Kamishna huyo ametaja
sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya
ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili
kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.
Kidata amesema kuwa katika
kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka
hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye
nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria
watakaobainika wamekwepa kodi.
Katika hatua nyingine Kaimu
Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni
11.8zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika
Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.
Amesema kuwa makusanyo hayo
yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara
19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao
wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao.