Ziara
ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15)
iliyoanzia kanda ya ziwa na kanda ya Magharibi kisha kuendelea katika
nchi za Rwanda, Uganda na Kenya mwezi huu imesitishwa kutokana na
kufungwa akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na Mamlaka ya
Mapato nchini (TRA).
Timu hiyo ya vijana iliondoka wiki
iliyopita kuelekea jijin Mwanza, ambapo iliagwa na kukabidhiwa bendera
ya Taifa na katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki
na timu ya Alliance kabla ya kuelekea mkoani Kigoma.
Ikiwa Kigoma U-15 ilicheza michezo
miwili ya kirafiki na timu ya kombaini ya mkoa wa Kigoma U-15, jumapili
ikacheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Burundi U-17, na jana
asubuhi kuanza safari ya kurejea jijini Dar essalaam.
Awali ziara ya timu hiyo ya U-15
ilikua iendelee katika mji wa Kigali kwa kucheza na U17 ya Rwanda,
Kampala kucheza na Uganda U17, jijini Nairobi kwa kucheza na U17 ya
Kenya na kumaliza ziara hiyo kwa kuchez ana U15 kombaini ya mkoa wa
Arusha Disemba 23, na kurejea jijin Dar es salaam Disemba 24, 2015.
U-15 inajiandaa na michuano ya
Viajana U17 kuwania kufuzu kwa Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini
Madagascar itakayoanza kutimua vumbi Juni 2016.