TANZANIA MWENYEJI KWENYE MAFUNZO YA KUKABIRIANA NA MATUKIO YA KINYUKLIA

December 08, 2015


Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Tume  ya Nguvu za Atomiki, Tanzania,  Dr. Mwijarubi Nyaruba aliekaa katikati pamoja na wataalamu wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya  namna ya kukabiliana na kuimarisha ulinzi wa matukio ya kinyuklia.

Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabirina na matukio ya mionzi hatari, mafunzo haya yatachukua siku nne na yameanza jana jumatatu tarehe 07 disemba na yatafika ukomo wake tarehe 10 disemba, 2015, mafunzo haya yana jumla ya washiriki 23 kutoka katika nchi sita za ukanda wa Afrika ikiwa ni Uganda, Kenya, Zimbabwe, Botswana, Ethiopia, Namibia na mwenyeji Tanzania mafunzo  yanalenga zaidi kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia endapo hakutakuwa na uangalizi wa kutosha.

Akifungua mafunzo haya jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Tanzania Dr. Mwijarubi Nyaruba amesema, kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu sana kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za atomiki duniani kuendelea kutoa mafunzo na kujadiliana jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi  ayonisha.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dr. Nyaruba aliendelea kufafanua kuwa kutokana na ongezeko la vitendo vya ugaidi duniani ni lazima kujiimarisha kwa namna yoyote ile ili kuweza kulinda vyanzo vyote vya mionzi vinavyotumika mahospitalini na sehemu zingine za viwanda pamoja na kuvitafuta vyanzo vya mionzi ambavyo vimetekelekezwa au kupotea (Orphan Sources) na kuvihifazi kwa umakini mkubwa vyanzo hivi hatari, visijie kuingia katika mikono ambayo sio salama na kutumika katika matukio ya kigaidi na kuleta athari kubwa kwa wananchi pamoja na mazingira kwa ujumla, hivyo ni jukumu la nchi wanachama kuendelea kubadilishana uzoefu ili kuweza kuzibiti vyanzo hivi.

Naye mshiriki kutoka Kenya , ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha kuzuia majanga, ndugu Pius Masai Mwachi amesema kuwa ni muda muhafaka sasa kwa nchi zote za jumuhiya ya afrika mashariki kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la namna ya kukabiliana na majanga yote yanayoweza kusababishwa na mabaki ya mionzi, kwani mionzi ni hatari sana na ni lazima kama nchi wanachama hasa waheshimiwa maraisi wa nchi hizi za jumuhiya ya adfrika mashariki kuweza kuhakikisha wanatoa kipaumbele kikubwa ili kuweza kukabiliana majanga yanayoweza kusababishwa kwa kutumia mabaki ya mionzi.

Mtaalamu mshiriki kutoka Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA Ndugu John Jones amesema kuwa dunia kwa ujumla inakabiliana na changamoto kubwa juu ya matukio mbalimbali ya kigaidi yanayoendelea duniani, hivyo Nchi zote wanachama ikiwepo Tanzania wana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa juhudi kubwa zinafanyika ili kuweza kukabiliana na hari yoyote hatarishi pindi matukio na majanga ya kinyuklia yanapoweza kutokea.

Tanzania Kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki imejenga jengo maaalumu la kuhifadhia mabaki ya mionzi Central Radioactive Waste Management Facility (CRWMF) ambapo vyanzo vyote vya mionzi vilivyokwisha nguvu kutoka mahospitalini, sehemu za tafiti pamoja na viwandani huchukuliwa na kusafirishwa kwa umakini mkubwa na kuhifadhiwa katika jengo hilo maalumu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »