Naibu
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto),
 akisalimiana na Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel Mgonja ,
 wakati wa  ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini jijini Dar 
es Salaam.  Wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, 
Sylvester  Ambokile.
 Kamishna
 Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester  Ambokile (kushoto), akimuonesha Naibu 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya 
Ofisi za Idara ya Uhamiaji, wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara 
katika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Naibu
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye 
tai),akipewa maelezo alipotembelea Dawati la Mapokezi wakati wa ziara ya
 kikazi aliyoifanya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji,Kurasini, jijijni 
Dar es Salaam.
 Afisa
 Uhamiaji, Lilian Maleko akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai), jinsi  taarifa za 
muombaji pasi ya kusafiria zinavyohakikiwa, wakati wa ziara ya kikazi 
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
 Afisa
 Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa hati za  kusafiria,  Amir 
Hassan (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye tai),moja ya pasi iliyokua 
imeshachapwa tayari kwa matumizi ya kusafiria, wakati wa ziara ya kikazi
 Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna
 wa Uhamiaji (Vibali vya Ukaazi, Visa na Pasi), Victoria Lembeli 
(katikati), akimuonesha  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani 
ya Nchi, John Mngodo, moja ya karatasi iliyokataliwa na mfumo wa komputa
 baada ya kubainika kwa taarifa za uongo za muombaji wa Hati ya Ukaazi, 
wakati Naibu Katibu Mkuu  huyo alipotembelea Makao Makuu ya Uhamiaji, 
Kurasini,jijini Dar es Salaam.
 Maafisa
 wa Idara ya Uhamiaji, wakimsikiliza  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya 
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani), alipofanya mkutano
 nao wakati wa ziara aliyofanya  Makao Makuu ya Uhamiaji,Kurasini, 
jijini Dar es Salaam.
Kamishna
 Jenerali wa Uhamiaji, Silvester Ambokile akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu 
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, baadhi ya machapisho 
ya Idara ya Uhamiaji, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea Makao 
Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Naibu
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (mwenye 
tai) katika picha ya pamoja na viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati 
alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es 
Salaam.  Wapili kushoto mstari wa mbele, ni Mkurugenzi wa Utawala na 
Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bi. 
Lilian Mapfa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
EmoticonEmoticon