Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani
Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi
hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi
cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari
na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.
Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka
hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri
hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo
chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha mfukuza kazi.
Watumishi wawili kati ya wanne
wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za
mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi
waliostaafu na wengine kuacha
kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi
walioacha kazi.
|
EmoticonEmoticon