Tigo yadhamini tamasha kubwa la muziki mikoa ya kusini

November 13, 2015

 Iringa, 13th Novemba 2015- Kampuni ya Tigo Tanzania imedhamini tamasha la muziki
kwa wanamuziki chipukizi katika mikoa ya Kanda ya kusini ikiwa ni fursa ya wasanii
hao  kuonesha vipaji vyao kwa wapenzi wa muziki.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tigo
Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, udhamini wa tamasha hilo liitwalo ‘Mtikisiko’ ni sehemu ya sera ya
kampuni hiyo ya kusaidia makundi mbalimbali katka kijamii wakiwemo vijana na
wasanii kufikia ndoto zao za kimaisha.
Akifafanua zaidi tamasha hilo Kiswaga,
alisema bonanza la Mtikisiko litakuwa
nyenzo ya kuwasaidia wanamuziki wapya kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe,
Ruvuma na Rukwa kwa kuwatambulisha mbele ya mashabiki na wapenzi hivyo kuwaweka
katika nafasi ya kujipatia kipato kutokana na kazi zao zao.
 “Udhamini huu umeonesha ni jinsi gani Tigo imedhamiria
kusaidia kuendeleza mikakati na shughuli mbalimbali za ubunifu zinayofanywa na
vijana katika harakati zao za kujiinua kiuchumi,” alisema Kiswaga.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema mapema
mwaka huu kampuni ya Tigo ilizindua huduma iitwayo Tigo Music ambayo inawapa
wanamuziki nchini fursa ya kupakia nyimbo zao kwenye mtandao wao Internet na hivyo
kuweza kusikilizwa na hadhira ya kitaifa na kimataifa jambo ambalo linawapa wasanii
kipato cha ziada na fursa ya kujulikana kimataifa.
“Jukwaa la Tigo Music limetoa
mchango  muhimu katika kuwanyanyua
wasanii wanaoibukia  na kuchangia kuibuka
kwa nyota wa ndani hadi kufikia viwango vya kimataifa. Ni matarajio yetu kwamba
Bonanza hili la Mtikisiko ambalo litakalofanyika
kwa kipindi cha wiki mbili litaibua majina na vipaji vipya katika Sanaa ya
muziki nchini,” alisema Kiswaga
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »