Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (kulia), akibadilishana Nyaraka za
Makabidhiano na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omari
Chambo (Kushoto). Maswi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Manyara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Omari Chambo (Kushoto), akisaini Nyaraka za
Makabidhiano sambamba na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Eliakim Maswi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa
Manyara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Omari Chambo (kulia) akipokea Shada la maua kutoka
kwa Mary Mkwaya Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, mara baada
yakuwasili wizarani. Wanaoshuhudia nyuma ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi
Paul Masanja na Mkurugenzi wa Utawalana RasilimaliWatu, Mrimia Mchomvu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Mhandisi Paul Masanja (kulia) akipokea shada la maua
kutoka kwa Cecilia Mrope Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Omari Chambo, akiongea jambo na Wajumbe wa
Menejimnenti wa Wizara baada ya kuwasili wizarani hapo. Katibu Mkuu
alitumia kikaohicho kuwaeleza wajumbe masuala muhimu ambayo atayasimamia
kikamilifu katika sekta za Nishati na Madini.
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akimpongeza, aliyekuwa
Kamishna wa Madini Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
…………………………………………………………………………….
- Makatibu wapya wataja vipaumbele
- Kuzingatia 4Us, Uendelezaji Wachimbaji Wadogo
Teresia Mhagama na Asteria Muhozya
Katibu Mkuu mpya na Naibu Katibu
Mkuu walioteuliwa kuiongoza Wizara ya Nishati na Madini wameanza
majukumu yao na kusisitiza watumishi wa Wizara na Taasisi zake
kuzingatia Uadilifu, Ubunifu, Uwajibikaji, na Uwazi katika utekelezaji
wa majukumu yao ya kila siku.
Wakizungumza na wajumbe wa
menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini, viongozi hao walisisitiza
baadhi ya masuala yatakuwa kipaumbele kuwa ni uwepo wa umeme wa
uhakika na bei nafuu ili wananchi watumie nishati hiyo kujiletea
maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Vipaumbele vingine ni kuongeza
mchango wa sekta madini katika pato la Taifa, uwepo wa kiwanda cha
kusindika gesi asilia, na suala la uwezeshaji wazawa (Local Content) katika sekta za Nishati na Madini.
Vilevile, vipaumbele vingine ni
kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanasaidiwa katika masuala ya fedha
na utaalam na kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari
Chambo, pamoja na kumshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Eliakim Maswi kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi
mkubwa, alitoa wito wa ushirikiano kati ya uongozi huo mpya na
wafanyakazi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi
Paul Masanja pamoja na kuainisha vipaumbele mbalimbali vya utekelezaji
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya
Kikwete kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kueleza kuwa, imetokana na
kuridhika na utendaji wake wa kazi wakati aliposhika nyadhifa mbalimbali
ikiwemo kuwa Kamishna wa Madini nchini.
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa
Wizara ya Nishati na Madini kutoa ushirikiano kwa uongozi huo ili kwa
pamoja waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katka
uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini.
Kabla ya kukabidhi nyaraka za
makabidhiano, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Eliakim Maswi
ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, aliwashukuru
watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa ushirikiano waliompa wakati
wa kipindi cha uongozi wake na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii na kutoa
ushirikiano kwa uongozi mpya.
Vilevile, aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu, Mhandisi Ngosi Mwihava ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Maji, aliwaasa Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa
kushirikiana, kuzingatia taratibu, sheria na kanuni, kuzingatia muda na
kuimarisha mawasiliano.
Kabla ya kushika nyadhifa hizi
Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara
na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja alikuwa Kamishna wa Madini
nchini.
EmoticonEmoticon