KING
of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’,akishirikiana na bendi
yake ya Malaika Music pamoja na Msaga Sumu na Kadjanito jana katika
usiku wa Idd el Hajj waliwapagawisha mashabiki vilivyo ndani ya Uwanja
wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini
Dar. Chipukizi watisha Katika usiku huo uliotambulika kama Usiku wa
Amerudi, pazia la burudani lilifunguliwa na chipukizi ambao walionesha
vipaji vya hali ya juu katika kuimba na kucheza. Chipukizi Small J,
aliwavuta mashabiki wengi kwa kuingia na staili iliyofananisha na staa
wa Bongo Fleva, Belle 9 na kufanya wengi wamshangilie.
Mbali
na hapo wapo chipukizi waliofunika kama vile Bad Spence, wakali wa
vinanda, na chipukizi mwenye asili ya kizungu kutoka Tongwe Records.
Pazia la chipukizi lilifungwa na msanii Galaxy ambaye aliingia kwa
mbwembwe na madensa wake waliofanya ukumbi wote uvutike na kushangaa
shoo ambayo mashabiki wengi hawakutegemea.
Wakali
Dancer watisha kwa kucheza Kundi la kucheza la Wakali Dancer liliingia
kwa mbwembwe ambapo lilianza kwa kucheza Wimbo wa Move Bit** na kufanya
jukwaa lote lilipuke kwa shangwe. Msaga Sumu akinukisha Bingwa wa muziki
wa Singeli asiye na mpinzani, Msaga Sumu aliingia na kufanya ukumbi
wote ulipukwe upya kwa shangwe.
Msaga
Sumu alianza kwa kuwapiga nyimbo zake zote kali kama vile Rafiki wa
Kweli kisha akafuatiwa na Naipenda Simba ambao ulifanya mashabiki wengi
wajiachie kwa kunyoosha mikono juu kwa muda mrefu. Msaga Sumu aliendelea
kukinukisha zaidi kwa kugonga vionjo vya Wimbo wa Huyo Mtoto kisha
akamalizia wimbo wenyewe ambapo mashabiki wengi walimtaka asishuke
jukwaani.
Kadjanito
awasisimua mashabiki Staa kutoka Jumba la Vipaji (THT), Kadjanito naye
alikuwa mmoja waliofunika ukumbini hapo. Kadja aliwaduwaza mashabiki
wengi kwa muonekano wake na kwakuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuzama
katika kiwanja hicho, iliwafanya mashabiki wengi wavutike na
kumshangilia kwa ikumshangaa. Staa huyo alianza kwa kuwatupia Wimbo wa
Maumivu Niache ambapo ukumbi wote ulikuwa ukiimba naye.
Baada
ya hapo aliangusha Wimbo wa Sina Maringo ambao wengi walikuwa wakicheza
naye jukwaani na kisha akamalizia Wimbo wa Nzogo ambao umechanganyikana
na lugha ya Kisukuma. Bella amaliza kila kitu Burudani ilihitimishwa na
King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ ambapo walianza
Malaika Music kwa kutoa bonge moja la sebene kisha akaingia Bella na
kuanza kuimba Wimbo wa Amerudi uliofanya mashabiki wengi wapige kelele.
Bella
aliamsha shangwe zaidi pale alipowaita wadada na kinamama wote kusogea
karibu kisha kunyoosha mkono na kuanza kuimba nao Wimbo wa Nani kama
Mama. Burudani iliendelea zaidi kwa Bella kwa kukamua nyimbo zake kibao
kama vile Nakuhitaji, Safari Siyo Kifo kisha akawamaliza kabisa
mashabiki kwa kupiga Wimbo wa Subira aliokuwa ameshirikisha na Cassim
Mganga.
STORI/PICHA: ISSA MNALLY, BONIPHACE NGUMIJE, GABRIEL NG’OSHA NA ANDREW CARLOS.
EmoticonEmoticon