MAHUJAJI WA 5 KUTOKEA TANZANIA WATHIBITISHWA KUFA HUKO MAKKA

September 25, 2015

WATU wasiopungua 700 wamekufa, huku wengine 816 wakijeruhiwa jana jirani na mji Mtakatifu wa Makka walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya nguzo muhimu katika Imani ya dini ya Kiislamu.
 
Kwa mujibu wa Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya mahujaji 2,000,000 waliokwenda Saudi Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka 
 
Tanzania.Kwa mujibu wa taarifa ya Sheikh Abu Bakari Zuberi Mufti wa Tanzania,  kwa vyombo vya habari amesema tayari wamethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine  wanne ni Watanzania.Amesema Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »