UPENDO NKONE KUZINDUA ALBAMU YA NYIMBO ZA INJILI YA “OMBA YESU ANASIKIA” JUMAPILI HII

September 25, 2015

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Upendo Nkone akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uzinduzi wa Albanu ya nyimbo kumi ikiwa mpaka sasa ametimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa nyia ya nyimbo hapa nchini.
 
 ALBAMU ya OMBA YESU ANASIKIA kuzinduliwa Septemba 27 mwaka huu(Jumapili hii) katika kanisa la TAG  la upanga mkabala na chuo cha Uzumbe kwa Askofu  Mwanesongore. 
 hayo yalisemwa na Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendio Nkone wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, alisema kuwa Mungu amemuokoa katika kifo ndio maana ameona aimbe kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na mambo aliyoyapitia, pia kumshukuru Mungu wa kutimiza miaka kumi ya kuinjilisha kwa njia ya Nyimbo.
Nkone alisema kuwa katika uzinduzi huo wa albamu ya OMBA YESU ANASIKIA kutakuwepo waimbaji wa nyimbo za Injili  ambao watatumbuiza katika uzinduzi wa albamu hiyo atakuwepo  Masanja mkandamizaji, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Kwaya ya Kijichi, Mather Baraka, Christina Matai, Mesi Chengula pamoja na Bendi.  
Pia alisema kuwa katika uzinduzi wa albamu hiyo kutakuwa na viingilio tofauti, watu wazima watalipia kiasi za shilingi elfu tano(5000) na watoto shilingi elfu mbili (2000).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »