Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa
aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi
Makaje Goso, wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam,
leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya
kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga
kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika leo jioni. Katikati ni Mke
wa Makamu wa Rais, Mama Zakia Bilal.
Picha zote na OMR
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akimfariji mke wa aliyekuwa
Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa Bin Simba, Bi Makaje Goso,
wakati alipofika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, leo Juni 16,
2015 kwa ajili ya kuifariji familia hiyo kabla ya kusafirisha mwili wa
marehemu kuelekea nyumbani kwake Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya maziko
yanayotarajia kufanyika leo jioni. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt.
Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika Kitabu
cha maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban
Issa Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni
jijini Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo
cha marehemu Simba.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akisaini katika Kitabu cha
maombolezo ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Marehemu Shaaban Issa
Bin Simba, wakati alipofika kwenye Ofisi za Bakwata, Kinondoni jijini
Dar es Salaam, leo Juni 16, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha
marehemu Simba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Aboud
Mohammed, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Ofisi za Bakwata,
Kinondoni kwa ajili ya kuhudhuria Kisomo cha Marehemu Simba, leo Juni
16, 2015. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan
Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na baadhi
ya Viongozi katika Kisomo cha kumuombea Marehemu Mufti Shaaban Bin
Simba, kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweny Viwanja vya Ofisi za
Bakwata zilizopo inondoni, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini
wa dini ya Kiislamu wakati wa Kisomo cha kumuombea marehemu Bin Simba,
kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kweye Viwanja vya Ofisi za Bakwata
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala
maalumu ya kuswalia Jeneza (halipo pichani) na baadhi ya viongozi wa
kitaifa wakati wa kisomo maalumu kilichofanyika leo Juni 16, 2015 kwenye
Viwanja vya Ofisi za Bakwata zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam,
kwa ajili ya kumuombea marehemu.
EmoticonEmoticon