KLABU ya African Sports “Wanakimanumanu”inatarajiwa
kuingia kambini Juni 3 mwaka huu kwa ajili ya kujiwinda na Michuano ya Ligi kuu
Tanzania Bara msimu ujao baada ya kupanda kucheza daraja hilo.
Akizungumza jana, Katibu wa timu hiyo, Khatib
Enzi aliliambia gazeti hili kuwa wameamua kuingia kambini mapema ili kuhakikisha
wanakiandaa vema kikosi chao kwa ajili ya kuhimili mikimiki ya Ligi kuu ikiwemo
kupata matokeao mazuri.
Enzi alisema kuwa wachezaji wa timu
hiyo waliopo nje ya mkoa wa Tanga kwa sasa watalazimika kutua mkoani hapa Juni
Mosi mwaka huu tayari kuungana na wenzao katika kambi yao itakayokuwepo Kata ya
Usagara jijini Tanga.
“Kuanza kambi mapema ni miongoni mwa mipango yetu ya kuhakikisha
tunakiandaa kikosi chetu vyema kwani Ligi kuu sio lelemama hivyo inahitajika
kujipanga vema “Alisema Enzi.
Katika hatua nyengie,Enzi alisema
kuwa usajili ambao wataufanya kabla ya kuanza michuano hiyo utakuwa ni katika nafasi
za mlinda mlango, kiungo wa kati na washambualiaji ambao tayari kamati ya
usajili ya timu hiyo imeshaanza kazi ya kuhakikisha nafasi hizo zinapata
wachezaji makini watakaoiletea maendeleo.
Alisema kuwa msimu ujao wamepania
kufanya usajili wa nguvu ambao utawawezesha kurudisha enzi zao za zamani wakati
walipopanda daraja na kuchukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Hata hivyo alisema kuwa klabu hiyo
imekwisha kuwafungashia virago wachezaji sita ambao ni Gerary Samburu, Khasim
Mkele, Eddy Zaharani, Nyanda Kazioba, Shingwa na Evarist Mujwahuki ambao wapo
huru.
EmoticonEmoticon