Mkazi
wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Esther Batolomea akisoma kipeperushi
chenye ujumbe wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza
maradhi hayo iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa
kushirikiana na Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia
kampeni inayozunguka mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake
wajitokeze wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani
ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa
kujifungua.
Wakazi
wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma wakisoma vipeperushi vyenye ujumbe
wa maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo
iliyofanyika wilayani hapo. Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na
Vodacom Foundation zinatoa elimu kwa Umma kupitia kampeni inayozunguka
mikoa mitatu nchini kuwasisitiza wanawake wajitokeze wakatibiwe maradhi
hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na
maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Wanafunzi
wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa
Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community
Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na
maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo
inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo
inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom
Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi
hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Balozi
wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba”
akitoa elimu kwa wakazi wa Kibonda kuhusiana na maradhi ya fistula na
kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani
yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na
Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo
inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa
wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.
EmoticonEmoticon