Naibu
wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango
akisisitiza jambo mbele ya Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
waliohudhuria Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na
chuo hicho jijini Dar es Salaam jana. Kwenye mkutano huo wa siku mbili
huku ukilenga kujadili masuala ya tafiti kwenye sayansi ya afya, Mh.
Kilango alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dr Mohamed Gharib Billal.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Anna Kilango (kulia) akijadiliana
jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya, mara baada ya ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo hicho jijini Dar
es Salaam jana.
Baadhi
ya wanasayansi, Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka Chuo Kikuu
Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakifuatilia kwa
umakini Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na chuo
hicho jijini Dar es Salaam jana
Naibu
wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi, Mh. Anne Kilango
amebainisha kuwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16
imeongeza fungu zaidi kwenye masuala ya utafiti hususani ule wa sayansi
ya afya.
Mh.
Kilango alitoa kauli jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua
Mkutano Mkuu wa tatu wa sayansi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu Cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kuhudhuliwa na mamia ya
Madaktari na wanafunzi wa udaktari kutoka chuo hicho.
“
Ili taifa liweze kufanya vizuri kwenye sekta yoyote ile ni lazima
tuwekeze zaidi kwenye masuala ya tafiti. Kwa kulitambua hilo napenda
kuwataarifu kuwa hata kwenye bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha tunatenga
kiasi kikubwa cha rasilimali fedha kwa ajili ya kuwezesha tafiti hizi
zikiwemo hizi za masuala ya afya,’’ alisema Mh. Kilango ambaye
alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr
Mohamed Gharib Billal.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili (MUHAS) Prof.Ephata Kaaya alisema kuwa kwa sasa taifa
linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya
kuambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na saratani.
“
Ni dhahiri kuwa kwa sasa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yamekuwa ni
tishio kwa taifa. Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuja tija
zaidi tukiwekeza katika tafiti zinazohusu pia magonjwa haya,’’
alibainisha.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuhitimishwa leo ambapo zaidi ya tafiti 100 kuhusu maswala ya afya zitawasilishwa.
EmoticonEmoticon