Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiwasilisha bajeti ya
wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Said Mtanda akiwasilisha mapendekezo ya
kamati yake kuhusu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakati wa bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kushoto)
akiwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka
kushoto) wakifuatilia kwa makini bajeti ya Wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini
Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO
……………………………………………….
Abraham Nyantori MAELEZO, Bungeni, Dodoma
Serikali imeshauriwa kutenga fedha
za kutosha ili kuiwezesha Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Ushauri huo umetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo
ya Jamii wakati wa kuwasilisha mapendekezo yake leo bungeni mjini
Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati Mhe. Said Mtanda amesema Wizara hiyo ina
jukumu la kuratibu na kusimamia maendeleo ya vijana, utamaduni, michezo
na habari hivyo ikipewa fungu la kutosha itaweza kuleta mabadiliko
chanya kwenye sekta hizo.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni leo Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara ameliomba
Bunge kuidhinisha bajeti ya wizara hiyo ya shilingi bilioni 29.4 ambapo
shilingi bilioni 5 ni kwa ajili ya maendeleo na shilingi bilioni 24.4 ni
matumizi ya kawaida.
Aidha Waziri Mukangara ameeleza jitihada mbalimbali
zinazofanywa na wizara yake zikiwemo kuratibu na kuwajengea vijana uwezo
wa kubuni mawazo bora ya kujiajiri, kuhamasisha halmashauri kutenga
asilimia 5 ya bajeti yao kuboresha mifuko ya vijana na kuhamasisha
uanzishaji wa SACCOS.
Katika mwaka wa fedha uliopita wa 2014/2015, Waziri Mukangara
amesema wizara yake ilitoa mafunzo kwa vijana 1550 katika kujenga dhana
ya kujiajiri, na jumla ya shilingi bilioni 2 zilikopeshwa kwa vikundi
mbalimbali vya vijana kote nchini.
Kwa upande mwingine Dkt Mukangara amesema wizara yake
imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo mradi wa Mawasiliano na kukamilisha
lengo la milenia la kubadili matumizi ya analojia kwenda dijitali, mradi
huo ulikamilika mwezi Aprili mwaka huu. Miradi mingine katika mwaka wa
fedha uliopita ilikuwa ni ya utafiti ukiwemo wa msamiati wa lugha za
jamii, utafiti wa majina fiche 1800 ya lugha za asili.
Wizara katika mwaka huu wa fedha imeahidi kuongeza ufanisi
ikiwemo kuongeza ajira kwa vijana, kulinda mazingira, kutoa habari,
kulinda mila na desturi kudumisha amani na mshikamano wa katika jamii ya
watanzania.
Leo ni siku ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na
Wizara ya Maliasili na Utalii ambazo zimewasilisha makadirio ya mapato
na matumizi ya wizara zao na hatimaye kuruhusu Bunge kuendelea
kuzijadili bajeti hizo.
/ mitambo ya kukodi TBC na uchaakavu wa majengo, madeni 3.2 /1.3 serikali.
Katika kipindi cha 2014/15 wizara ipanga kukusanya sh.
1,149,008,000 kutoka vyanzo mbalimbali zilizokusanywa ni sh. 811,616,116
sawa 71%
Wizara ilitengewa (2014/2015) 19,806,611,000 zilipokelewa sh.
14,446,963,490 sawa na 73% ya bajeti ya matumizi ya kawaida. Fedha za
maendeleo wizara 2014/15 ilitengewa 16,850,000,000 ilipokea hadi april
2015 >7,000,000,000 sawa 42% upanuzi wa usikivu wa shirika la
utangazaji la Tanzania TBC
Moja ya changamoto ni kuongezeka kwa mifumo na njia za
mawasiliano kwa umma kama mitandao ya jamii kwenye intanet kunakoadhiri
maudhui ya taarifa zinazotolewa
Wizara kukabiliana na changamoto hizo imetoa elimu na kutembelea vituo kwa kushirikia na kamati ya maudhui (TCRA)
EmoticonEmoticon