CHADEMA KANDA YA KASKAZINI KUENDESHA OPERATION

May 25, 2015
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini
(CHADEMA), Amani Golugwa katikati akizungumza na waandishi wa habarijana kuhusu uzinduzi wa Operation maalumu ya kuwahimiza wananchikujiandikisha BVR itakayoongozwa na Mbunge wa Arusha mjini,GodblessLema kushoto ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Tanga,Ismail Masoud na kulia
ni Katibu wa Chama hicho wilaya ya Tanga,Azizi Lali

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini
(CHADEMA), Amani Golugwa akimkabidhi vitendea kazi,Afisa Kanda Mkazi wa Mkoa wa Tanga Chadema ,Jonathani Baweje mara baada ya uteuzi wake
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo kinatarajiwa kuzindua Operation kubwa ya kuhamasisha wananchi wa kanda ya Kaskazini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu Mpiga kura pindi litakapoanza ili waweze kupata haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza leo, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema operationi hiyo itakwenda sambamba na kuwaelimisha wananchi ili waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kutoka kanda ya Kaskazini waweze kushiriki.

Amesema kuwa kabla ya kuanza uzinduzi huo watafanya kongamano kubwa ambalo litawashirikisha wananchi walioonyesha nia ya kugombea nafasi kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga.

Golugwa amesema kuwaoparesheni hiyo itaongozwa na Mbunge wa Arusha Goodbless Lema ambaye baada ya uzibduzi huo anatarajiwa kufanya ziara za kuzunguka majimbo 33 yaliyoko kwenye kanda hiyo.


Katika hatua nyingine Golugwa alisema kuwa CHADEMA kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutafuta wagombea wanafasi mbalimbali za uchanguzi wakishirikiana na UKAWA katika maeneo mbalimbali .

Amesema kuwa wamekubaliana na vyama vinavyounda UKAWA kuhakikisha wanagawana majukumu katika maeneo ambayo wanafanya vizuri ilikuhakikisha wanashinda katika changuzi zinazokuja.

Kwa upande wa UKAWA hatugawani majimbo kama ilinavyoelezwa bali tumekubaliana kugawana majukumu katika maeneo ambayo chama kimoja kinaushawishi mkubwa ili kuweza kufanya vizuri.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »