Katibu
Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo
(RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, mashine 2 za
kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Kituo
hicho chenye Makao Makuu yake Jijini Nairobi. Halfa hii ilifanyika
katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo
(RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akitoa maelezo jinsi
mashine za kuweka alama silaha zinavyofanya kazi. Katikati ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na
kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.
Mashine
za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi
la Polisi Tanzania. Uwekaji wa alama katika silaha utasaidia udhibiti wa
matumizi ya silaha hapa nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akitoa
hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias
Chikawe kushukuru msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali ya Marekani
kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest Mangu akishukuru kuhusu msaada wa
mashine za kuweka alama silaha zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa
Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha
Ndogondogo, Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa nne
kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu (wa tatu toka kulia) na Katibu
Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo
(RECSA) Bw. Theoneste Mutsindashyaka (wa nne toka kushoto) baada ya
hafla ya kupokea mashine za kuweka alama silaha iliyofanyika katika
Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wengine ni Viongozi wa
Jeshi la Polisi Makao Makuu na wageni wengine waalikwa.
EmoticonEmoticon