Mkurugenzi
wa Maendeleo ya nUtamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akiwa katika maandanano ya
kuadhimisha siku ya Uanuai wa Utamaduni Dunia jijini Dar es Salaam juzi
ambapo maaandamano hayo yalianzia katika viwanja vya maonyesho ya
Biashara vya Mwalimu Nyererere Sabasabasa kupitia mtongani kwa Aziz Aly
na kurudi kiatika viwanja hivyo.Kulia ni balozi wa India nchini
Mhe.Debnath Shaw.
Baadhi
ya vikundi vya sanaa na wananchi wakiwa katika maandamano ya
kuadhimisha siku ya uanuai wa Utamaduni Dunia maandamano hayo yalianzia
katika viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Mwalimu Nyererere
Sabasabasa jijini Dar es Salaam kupitia mtongani kwa Aziz Aly na kurudi
kiatika viwanja hivyo.Siku hiyo ya Uanuai wa Utamaduni uadhimishwa
tarehe 21 May kila mwaka Duniani kote ikiwa na lengo la kukukuza na
kuibua kazi za sanaa na utamaduni.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline
Maleko akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai
wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar
es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa
Hermas Mwansoko na wa mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania
Bw. Debnath Shaw.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko Mkurugenzi kizungumza
wakiti wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni
Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi.
Jacqueline Maleko na mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania
Bw. Debnath Shaw.
Wapiga
vyombo vya muziki na ngoma kutoksa kikundi cha Tanzania wkichakarika
wakati wa zoezi la kutumbia kwenye hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya
siku ya uanuai wa Utamaduni.
Wanakikundi
cha sanaa kutoka nchini India wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniaa ambayo nufanyika kila tarehe 21 mwezi
wa tano kila mwaka.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Profesa Hermsa Mwansoko akicheza Bao na Balozi wa India nchini
Bw. Debnath Shaw wakati wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni
Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo
yameambatana na maonyesho ya wajisariamali wa bidhaa za kiutamaduni na
kuratibiwa kwa ushirikianao baiona ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni
na Tan Trade.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya nUtamaduni KUTOKA Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akiwa akiangalia namna wanafunzi wa
shule
…………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Wadau mbalimbali wa sekta ya Utamaduni nchini wameiomba jamii
kuuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa kuzingatia matumizi ya vitu
vinavyoendana na tamaduni za Tanzania ili kudumisha na kuenzi mila na
desturi za Tanzania.
Kauli hiyo imeibuliwa na wadau wa sekta ya Utamaduni
walioshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa
Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 21 ya mwezi Mei ambapo
Tanzania imeadhimisha siku hiyo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere
Sabasaba jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi. Jacqueline Maleko
ameiomba serikali kujenga kituo cha Utamaduni kitakachotumika
kuendeleza, kudumisha na kuhamasisha matumizi ya vitu vya asili ya
Tanzania hivyo kuendeleza tamaduni zetu.
“Utamaduni wa mtanzania ni urithi wenye mashiko kama utadumishwa
na kuhamasisha jamii kutumia vitu vya asili kama vile nyimbo, ngoma,
uchongaji, mashahiri, uchoraji, filamu Sanaa, vyakula na mavazi kwa
kuviendeleza na kuvinadi ndani na nje ya Tanzania” Amesema Bibi Maleko.
Akitoa maoni yake kuhusu utamaduni wa Tanzania Mwalimu Gasper
Maro kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa shule za msingi
zimekuwa zikijitahidi kuuenzi utamaduni wa Tanzania kwa kuwahamasisha
wanafunzi kuimba nyimbo za jadi na kucheza ngo ma za makabila mbalimbali
ili kuweza kujua tamaduni za kila kabila lililopo nchini Tanzania,
Hata hivyo mwalimu Maro amesema kuwa utamaduni wa Tanzania kwa
sasa unashuka kutokana na kizazi cha sasa kuiga tamaduni za nchi
nyingine na kudharau tamaduni zao hivyo kuwaomba maafisa utamaduni
nchini kuandaa programu mbalimbali zitakazokuwa zikihamasisha jamii
kuishi kwa kufuata tamaduni za Tanzania.
Kwa upande wake mwanafunzi Agustino George Pius kutoka Shule ya
Msingi Magomeni amesema kuwa utamaduni wa Tanzania umekua ukibadilishwa
na vijana kutokana na maendeleo ya teknolojia hasa katika upande wa
mavazi, vyakula, pamoja na staili ya maisha wanayoishi vijana wa sasa.
Naye Afisa Utumishi kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania
(COSOTA) Bw. Elius Ngemela ameitaka jamii kutambua kuwa utamaduni ni
utambulisho wa nchi ambao kama utatumika vizuri utasaidia kukuza uchumi
wa nchi na kutoa ajira katika jamii hivyo kuuthamini na kuudumisha kwa
maendeleo ya nchi yetu.
EmoticonEmoticon