Bayport yazindua
huduma mpya ya mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaama
KATIKA hali
isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya
Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na
kampuni nyingi kupewa mikopo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mwishoni
mwa wiki katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa
Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema kuwa ni kusudio lao kutoa fursa ya watumishi
wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali kupata nafasi ya kutimiza
ndoto za kumiliki ardhi nchini Tanzania.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Kibaha, Obed Katonga, kulia akijadiliana jambo na Meneja Uzalishaji wa Bayport Financial Services, Mashaka Mgeta kulia kwake na Mkuu wa Kanda ya Pwani, David Ndiega.
“Huduma yetu
katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana katika
matawi yote ya Tanzania Bara, ambapo kwenye matawi yetu yote fomu hizo zitakuwapo, huku fomu hizo za kukopeshwa viwanja zikipatikana kwa wiki mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.
“Si lazima
uwe mtumishi wa umma ili uwe na sifa ya kukopeshwa viwanja, ila hata
wajasiriamali nao wamekumbukwa katika huduma hii nzuri kwa Watanzania wote,
hivyo ni wakati wao sasa kuiunga mkono taasisi hii ili iweze kuwakomboa na
kuwakwamua pia,’ alisema Mbaga.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda mwenye shati jeupe mbele akiwa katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana jijini Dar es Salaam. Mwenye miwani ni Ruth Bura, mtumishi wa taasisi hiyo anayehusika na mambo ya Bima.
Akimwakilisha
Mkuu wa wilaya ya Kibaha katika uzinduzi huo, Afisa Mipango wa wilaya hiyo,
Obed Katonge, alisema kwamba Bayport imebuni huduma nzuri inayofaa kuungwa
mkono na Watanzania wote, hasa kwa kuingia kwenye sekta ya ardhi inayopanda
thamani siku hadi siku duniani kote.
Wadau wanafuatilia uzinduzi huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akiendelea kufafanua katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kushoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali.
Meneja Masoko wa Property International, Zora Moore, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, huku wao wakiwa ni kampuni iliyohusika na upimaji wa viwanja hivyo vya Vikuruti, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
Mambo yamekwenda poa. Ndivyo wanavyoonekana kusema Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga kulia na Meneja Masoko wake na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Clouds Tv na Radio, Salehe Masoud, akibadilishana mawazo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, mwenye shati jeupe na Mwandishi wa redio ya Times FM, Phillip Daudi.
Staff wa Bayport Financial Services wakijadiliana katika uzinduzi wa huduma yao.
Wadau wanafuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea katika uzinduzi huo.
Baada ya kuzindua, wadau walikuwa wakibadilishana mawazo kama hivi.
“Serikali
hususan kwenye wilaya yetu ya Kibaha tumepokea huduma hii kwa mikono miwili,
ukizingatia kuwa wilaya yetu ni kati ya maeneo yanayokuwa kwa kasi, hivyo
tunaamini tutaendelea kushirikiana na Bayport kwa ajili ya kuwapatia mwangaza
wateja na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Katonge.
Habari; napenda kuiwasilisha kwako stori ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka Bayport Financial Services, yenye maskani yake, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Wageni mbalimbali walialikwa akiwamo Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulifanyika jana ijumaa ya Mei 22 katika Hoteli ya Serena. Tunaomba sapoti yako ili Watanzania waone na waweze kuchangamkia fursa hii ya mikopo ya viwanja kutoka mradi wa vikuruti, uliopo Kibaha.
Kambi Mbwana, +255 71205949
Naye Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema
kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya ni njia ya kunapanua wigo wao na shabaha
ya kuwafaidisha wateja wao na Watanzania wote kwa huduma na bidhaa
zilizothibitishwa kwa ubora zaidi. “Bayport ilikaa na kufanya tafiti kadhaa zenye nia ya
kujenga jamii na kuinua uchumi wa Watanzania wote, hivyo tukaona ipo haja ya
kufungua ukurasa huu wa kukopesha viwanja, huku wateja wetu wakitakiwa kulipa
kila mwezi katika vipindi vya miezi 24, ambapo kiwanja cha chini kabisa
kinapatikana kwa Sh 1,700,000 na nzuri zaidi wateja wetu wanaweza kuona huduma
nyingine nzuri za mikopo kwa kupitia tovuti yetu ya www.kopabayport.co.tz ,”
alisema Cheyo.
Naye Meneja
Bidhaa wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema makato ya kiwanja
chenye thamani ya Sh 1,400,000 kwa mjasiriamali ni 105,181.55, wakati mtumishi
wa umma akilazimika kukatwa Sh 73,684.49, huku akiongeza kuwa mtu anaweza kupata
kiwanja kwa malipo ya fedha taslimu. “Naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi
kukopeshwa viwanja hivi ili watimize ndoto zao za ujenzi wa nyumba, maana
Bayport imekuja kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania wote, maana tangu
sasa kila mtu anaweza kuwa baba au mama mwenye nyumba,” alisema Cheyo.
Mbali na
huduma ya mkopo wa viwanja, Bayport pia inatoa mikopo mbalimbali ya bidhaa,
mikopo ya fedha taslimu, bima ya elimu kwa uwapendao, huku mikopo yote hiyo
ikiweza kupatikana kwa njia ya mtadao wa www.kopabayport.co.tz.
Click here to Reply, Reply to all, or Forward
6.07 GB (40%) of 15 GB used
Manage
Terms - Privacy
Last account activity: 1 hour ago
Details
22 more
Kambi Mbwana's profile photo
Kambi Mbwana
Recent photos
View photo in message
View photo in message
View photo in message
Show details
Compose:
New Message
MinimizePop-outClose
To
EmoticonEmoticon