Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga,mikoa yote
kanda ya ziwa na mashabiki wetu wote walioko nchi nzima na sehemu
mbalimbali duniani kwa kutoa ushirikiano wao wa dhati kwetu katika
michezo yetu ya ligi kuu tanzania bara msimu wa mwaka 2014-2015
iliomalizika tarehe 9/05/2015.
Tunasema asanteni sana kwa
michango yenu ya hali na mali,kifedha,kimawazo na ushauri pia,na hasa
katika kipindi kigumu ambacho tumepitia.
ulikuwa ni msimu wetu wa
kwanza kushiriki katika ligi mengi tumejifunza na kuona mazuri na magumu katika ligi hii
na soka la tanzania kwa ujumla,tunaahidi kuiandaa timu kwa wakati
muafaka na kwa weledi mkubwa lengo likiwa ni kufanya vizuri zaidi katika
msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara.
Tunasisitiza kuwa bado
hatujaanza kushughurika na swala la usajili wa mchezaji kwasasa na wala
hatujafanya mazungumza na mchezaji yoyotekuhusu kumsajili, tunasubiri
ripoti ya mwalimu wetu Mathias
Rule kujua anapendekeza tufanye nini katika kuboresha timu yetu.
Tunakanusha vikali Taarifa ambazo zinasambaa hivi sasa kuwa tunafanya au tumefanya
mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili kuwasajili akiwemo Juma Kaseja na Beki wa mtibwa
sugar Salim Mbonde hatuna mazungumzo na wachezaji hao na hatutafanya
usajili wowote bila kupata ripoti ya mwalimu.
kama ripoti ya
mwalimu itaelekeza tufanye usajili tutafanya hivyo na uongozi umejipanga
kufanya usajili wenye tija na umakini wa kutosha kwa manufaa ya timu
yetu ya Stand United fc.
Imetolewa na Idara ya Habari Stand United Fc.
Isaac Edward
Afisa habari.
Afisa habari.
0759 11 34 54
EmoticonEmoticon