Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa
jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi
wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee
ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya
sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog)
Umati
mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono Waziri mkuu
mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh
mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika
hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana
katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya
sh,200 milioni zilipatikana
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla
ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa
jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na
baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu
katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya
kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee.
Taswira
ya picha wakati Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli
mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti
mkubwa jijini Arusha.
Msafara wa pikipiki
Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa.
……………………………………………………………………….
Waziri mkuu mstaafu na
mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia
kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka
huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Lowasa,alitoa kauli
hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi
ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200
milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.
Akizungumza katika
hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu
anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku
hiyo.
“Niseme neno
nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku
hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji
mniunge mkono “alisema Lowasa
Lowasa kwa kujiamini
aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na
kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
“Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini”alisisitiza Lowasa
Hatahivyo,Lowasa
aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu
wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu
kusimamia amani ya mkoa huo.
Aliipongeza kamati hiyo na
kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa
kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.
“Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya
dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha
kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii
Arusha”alisema Lowasa na kuibua shangwe
EmoticonEmoticon