CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAAHIRISHA VIKOA VYA HALMAHAURI KUU NA KAMATI KUU

May 16, 2015

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habar katika ofisi za CCM makao  makuu jijini Dar es salaam wakati akizungumzia kusogezwa mbele kwa vikoa vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2 
Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wakati wa mkutano huo. 3 
Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………………………….
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeahirisha vikao vya Kamati kuu na Halmashauri kuu ya chama hicho vilivyotakiwa kuanza Mei 20 hadi 22 ,mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Katibu wa Nec,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,amesema sababu ya kuahirisha vikao hivyo ni kupisha ratiba ya vikao vya baraza la wawakilishi vitakavyoanza Mei 18 mwaka huu.
”Vikao vya baraza la wawakilishi vitaanza Mei 18 hadi 21,vikao hivi ambavyo vitafanyika mfululizo vitatoa ratiba ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais wa Zanzibar,Wabunge na Baraza la Uwakilishi,”amesema Nape
Nape alisema ratiba hiyo itawezesha wagombea kujitangaza na kuchukua fomu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »