Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF, limesema taarifa iliyoandikwa na Gazeti
moja la tarehe 15, Mei 2015 yenye kichwa cha habari “Nkurunziza ameweka
picha mbaya katika soka” haina uhusiano na TFF.
Katika
taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael
Bundala amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa
nchini Burundi.
TFF
imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli
hii ni mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF
unafuatilia ili kujua ni hatua gani zichukuliwe.
Jukumu la TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si vinginevyo.
TFF inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na baraka katika nchi yao.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania
EmoticonEmoticon